Matthew 15:30 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Watu wengi sana wakamjia wakiwaleta vilema, vipofu, viwete, bubu na wengine wengi waliokuwa wagonjwa, wakawaweka mbele ya miguu yake, naye Yesu akawaponya.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Umati mkubwa wa watu wakamjia, wakiwaleta vilema, vipofu, viwete, bubu na wengine wengi, wakawaweka miguuni pake; naye akawaponya.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wakamwendea makutano mengi wakimletea viwete, vipofu, mabubu, vilema, na wengine wengi, wakawaweka miguuni pake; akawaponya;
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kundi kubwa la watu likamwendea. Walileta watu wengine wengi waliokuwa wagonjwa na kuwaweka mbele yake. Walikuwepo watu wasioweza kutembea, wasiyeona, walemavu wa miguu, wasiyesikia na wengine wengi.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Watu wengi sana wakamjia wakiwaleta vilema, vipofu, viwete, bubu na wengine wengi waliokuwa wagonjwa, wakawaweka mbele ya miguu yake, naye Yesu akawaponya.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Watu wengi sana wakamjia wakiwaleta vilema, vipofu, viwete, bubu na wengine wengi waliokuwa wagonjwa, wakawaweka mbele ya miguu yake, naye Yesu akawaponya.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Umati mkubwa wa watu ukamjia, wakiwaleta vilema, vipofu, viwete, bubu na wengine wengi, wakawaweka miguuni pake, naye akawaponya.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Umati mkubwa wa watu ukamjia, wakiwaleta vilema, vipofu, viwete, bubu na wengine wengi, wakawaweka miguuni pake; naye akawaponya.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wakamwendea makutano mengi wakimletea viwete, vipofu, mabubu, vilema, na wengine wengi, wakawaweka miguuni pake; akawaponya;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Watu wengi sana wakamjia wakiwaleta vilema, vipofu, viwete, bubu na wengine wengi waliokuwa wagonjwa, wakawaweka mbele ya miguu yake, naye Yesu akawaponya.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wakamjia makundi mengi ya watu walio na viwete na wenye vilema na vipofu na mabubu na wengine wengi pamoja nao. Wakawaweka miguuni pa Yesu, naye akawaponya.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wakamwendea makutano mengi wakimletea viwete, vipofu, mabubu, vilema, na wengine wengi, wakawaweka miguuni pake; akawaponya;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Halafu makundi mengi ya watu wakamufikia, wakimuletea vilema, vipofu, viwete na wabubu. Wakawaweka mbele ya Yesu, naye akawaponyesha.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Wakamwendea makutano mengi walio na viwete, vipofu, bubu, vilema, na wengine wengi pamoja nao, wakawaweka miguuni pa Yesu; akawaponya;