Matthew 15:33 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wanafunzi wakamwambia, “Hapa tuko nyikani; tutapata wapi chakula cha kuwatosha watu wengi hivi?”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wanafunzi wake wakasema, “Tutapata wapi mikate ya kutosha kulisha umati mkubwa namna hii, nasi tuko nyikani?”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wanafunzi wake wakamwambia, Tupate wapi mikate mingi hapa nyikani, hata kushibisha mkutano mkuu namna hii?
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Wafuasi wakamwuliza Yesu, “Tutapata wapi mikate ya kutosha kuwalisha watu wote hawa? Tuko nyikani mbali ni miji.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Wanafunzi wakamwambia, “Hapa tuko nyikani; tutapata wapi chakula cha kuwatosha watu wengi hivi?”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wanafunzi wakamwambia, “Hapa tuko nyikani; tutapata wapi chakula cha kuwatosha watu wengi hivi?”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wanafunzi wake wakasema, “Tutapata wapi mikate ya kutosha kuwalisha umati huu wa watu mkubwa namna hii, nasi tuko nyikani?”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wanafunzi wake wakasema, “Tutapata wapi mikate ya kutosha kuwalisha umati huu wa watu mkubwa namna hii, nasi tuko nyikani?”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wanafunzi wake wakamwambia, Tupate wapi mikate mingi hapa nyikani, hata kushibisha mkutano mkuu namna hii?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wanafunzi wakamwambia, “Hapa tuko nyikani; tutapata wapi chakula cha kuwatosha watu wengi hivi?”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wanafunzi wakamwambia: Hapa nyikani tutapata wapi mikate inayotosha kuwashibisha watu walio wengi kama hawa?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wanafunzi wake wakamwambia, Tupate wapi mikate mingi hapa nyikani, hata kushibisha mkutano mkuu namna hii?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nao wanafunzi wake wakamujibu: “Hapa katika pori, tutaweza kupata wapi chakula cha kushibisha kundi kubwa kama hili?”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Wanafunzi wake wakamwambia, Tupate wapi mikate mingi hapa nyikani, hatta kushibisha makutano mengi namna hii?