Matthew 15:36 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Akaitwaa ile mikate saba na vile visamaki, akamshukuru Mungu, akavimega, akawapa wanafunzi, nao wakawagawia watu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha akachukua ile mikate saba na wale samaki, naye akamshukuru Mungu, akavimega na kuwapa wanafunzi wake, nao wakawapa watu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
akaitwaa ile mikate saba na vile visamaki, akashukuru akavimega, akawapa wanafunzi wake, nao wanafunzi wakawapa makutano.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Akaichukua mikate saba na samaki. Akamshukuru Mungu kwa sababu ya chakula. Akaigawa vipande vipande, akawapa wafuasi wake na wafuasi wakawapa watu chakula.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Akaitwaa ile mikate saba na vile visamaki, akamshukuru Mungu, akavimega, akawapa wanafunzi, nao wakawagawia watu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Akaitwaa ile mikate saba na vile visamaki, akamshukuru Mungu, akavimega, akawapa wanafunzi, nao wakawagawia watu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha akachukua ile mikate saba na wale samaki, naye akiisha kumshukuru Mungu, akavimega na kuwapa wanafunzi wake, nao wakawapa ule umati wa watu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha akachukua ile mikate saba na wale samaki, naye akiisha kumshukuru Mungu, akavimega na kuwapa wanafunzi wake, nao wakawapa ule umati wa watu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
akaitwaa ile mikate saba na vile visamaki, akashukuru akavimega, akawapa wanafunzi wake, nao wanafunzi wakawapa makutano.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Akaitwaa ile mikate saba na vile visamaki, akamshukuru Mungu, akavimega, akawapa wanafunzi, nao wakawagawia watu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha akaitwaa ile mikate saba na samaki, akashukuru, akaimega akawapa wanafunzi, nao wanafunzi wakawapa wao wa makundi ya watu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
akaitwaa ile mikate saba na vile visamaki, akashukuru akavimega, akawapa wanafunzi wake, nao wanafunzi wakawapa makutano.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha akatwaa ile mikate saba na zile samaki, akamushukuru Mungu, akaimega na kuwapa wanafunzi wake wavigawanye kwa watu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
akaitwaa ile mikate saba na vile visamaki, akashukuru, akavimega, akawapa wanafunzi wake, nao wanafunzi wakawapa makutano.