Matthew 15:4 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mungu amesema: ‘Waheshimu baba yako na mama yako,’ na ‘Anayemtukana baba yake au mama yake, lazima auawe.’
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa maana Mungu alisema, ‘Waheshimu baba yako na mama yako,’ na, ‘Yeyote amtukanaye baba yake au mama yake, na auawe.’
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa kuwa Mungu alisema, Mheshimu baba yako na mama yako, na Amtukanaye baba yake au mama yake kufa na afe.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mungu alisema, ‘Ni lazima umtii baba na mama yako.’ Na Mungu alisema pia kuwa, ‘Kila anayemnenea vibaya mama au baba yake lazima auawe.’
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mungu amesema: Waheshimu baba yako na mama yako, na Anayemkashifu baba yake au mama yake, lazima auawe.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mungu amesema: ‘Waheshimu baba yako na mama yako,’ na ‘Anayemtukana baba yake au mama yake, lazima auawe.’
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa maana Mungu alisema, ‘Waheshimu baba yako na mama yako’ na ‘Ye yote amtukanaye baba yake au mama yake, na auawe.’
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa maana Mungu alisema, ‘Waheshimu baba yako na mama yako,’ na, ‘Yeyote amtukanaye baba yake au mama yake, na auawe.’
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa kuwa Mungu alisema, Mheshimu baba yako na mama yako, na Amtukanaye baba yake au mama yake kufa na afe.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mungu amesema: ‘Waheshimu baba yako na mama yako,’ na ‘Anayemtukana baba yake au mama yake, lazima auawe.’
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kweli Mungu alisema: Mheshimu baba yako na mama yako! na tena: Atakayemwapiza baba au mama sharti afe kwa kuuawa!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa kuwa Mungu alisema, Mheshimu baba yako na mama yako, na Amtukanaye baba yake au mama yake kufa na afe.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa maana Mungu alisema: ‘Uwaheshimu baba yako na mama yako.’ Naye alisema vilevile: ‘Anayelaani baba yake au mama yake anapaswa kuuawa.’
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kwa kuwa Mungu aliamuru, akisema, Mheshimu baba yako na mama yako; na, Amtukanae baba yake au mama yake na afe.