Matthew 15:5 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini nyinyi mwafundisha ati mtu akiwa na kitu ambacho angeweza kumsaidia nacho baba yake au mama yake, lakini akasema: ‘Kitu hiki nimemtolea Mungu,’
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini ninyi mwafundisha kwamba mtu akimwambia baba yake au mama yake, ‘Kile ambacho ningeweza kukusaidia kimewekwa wakfu kwa Mungu,’
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Bali ninyi husema, Atakayemwambia babaye au mamaye, Cho chote kikupasacho kusaidiwa na mimi ni wakfu,
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Lakini mnafundisha kuwa mtu anaweza kumwambia baba au mama yake, ‘Nina kitu ninachoweza kukupa kukusaidia, Lakini sitakupa, bali nitampa Mungu.’
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Lakini ninyi mwafundisha ati mtu akiwa na kitu ambacho angeweza kuwasaidia nacho baba au mama yake, lakini akasema: Kitu hiki nimemtolea Mungu,
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini nyinyi mwafundisha ati mtu akiwa na kitu ambacho angeweza kumsaidia nacho baba yake au mama yake, lakini akasema: ‘Kitu hiki nimemtolea Mungu,’
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini ninyi mwafundisha kwamba mtu akimwambia baba yake au mama yake, ‘Kile ambacho ningeweza kukusaidia kimewekwa wakfu kwa Mungu,’ basi hana tena sababu ya kumsaidia baba yake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini ninyi mwafundisha kwamba mtu akimwambia baba yake au mama yake, ‘Kile ambacho ningeweza kukusaidia kimewekwa wakfu kwa Mungu,’
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Bali ninyi husema, Atakayemwambia babaye au mamaye, chochote kikupasacho nikusaidie kwacho nakitoa wakfu,
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini nyinyi mwafundisha ati mtu akiwa na kitu ambacho angeweza kumsaidia nacho baba yake au mama yake, lakini akasema: ‘Kitu hiki nimemtolea Mungu,’
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini ninyi husema: Mtu akimwambia baba au mama: Mali, unazozitaka, nikusaidie nazo, amepewa Mungu, basi, ni vema.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Bali ninyi husema, Atakayemwambia babaye au mamaye, Cho chote kikupasacho kusaidiwa na mimi ni wakfu,
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini ninyi munasema kwamba mutu akiwa na kitu ambacho angeweza kuwasaidia baba yake au mama yake, lakini akimwambia kwamba amekitoa sadaka kwa Mungu,
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bali ninyi hunena, Afakaemwambia baba yake au mama yake, Cho chote kikupasacho kufaidiwa nami ni sadaka, asimheshimu baba yake au mama yake, huwa bassi.