Matthew 16:18 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nami nakuambia: Wewe ni Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala nguvu za kifo hazitaweza kulishinda.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nami nakuambia, wewe ndiwe Petro na juu ya mwamba huu nitajenga jumuiya ya wafuasi wangu, hata malango ya Kuzimu hayataweza kuwashinda.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Hivyo ninakwambia, Wewe ni Petro. Na nitalijenga kanisa langu kwenye mwamba huu. Nguvu ya mauti haitaweza kulishinda kanisa langu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Nami nakwambia: wewe ni Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala kifo chenyewe hakitaweza kulishinda.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nami nakuambia: wewe ni Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala nguvu za kifo hazitaweza kulishinda.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nami nakuambia, wewe ndiwe Petro na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu, hata malango ya kuzimu hayataweza kulishinda.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nami nakuambia, wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitajenga jumuiya ya wafuasi wangu, hata malango ya Kuzimu hayataweza kuwashinda.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nami nakuambia: Wewe ni Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala nguvu za kifo hazitaweza kulishinda.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nami nakuambia: Wewe ndiwe Petero, juu ya mwamba huu nitalijenga kundi la wateule wangu, nayo malango ya kuzimu hayatawashinda.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nami sasa ninakuambia: ewe Petro, wewe ni jiwe, na juu ya jiwe hili, nitajenga musingi wa kanisa langu, na hata uwezo wa lufu hautaweza kulishinda.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na jun ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; na milango ya kuzimu haitalishinda.