Matthew 16:23 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini Yesu akageuka, akamwambia Petro, “Ondoka mbele yangu, Shetani! Wewe ni kikwazo kwangu. Mawazo yako si ya kimungu ila ni ya kibinadamu!”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini Isa akageuka na kumwambia Petro, “Rudi nyuma yangu, Shetani! Wewe ni kikwazo kwangu. Moyo wako hauwazi yaliyo ya Mungu, bali ya wanadamu.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akageuka, akamwambia Petro, Nenda nyuma yangu, Shetani; u kikwazo kwangu; maana huyawazi yaliyo ya Mungu, bali ya wanadamu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ndipo Yesu akamwambia Petro, “Ondoka kwangu, Shetani! Hunisaidii! Hujali mambo ya Mungu. Unajali mambo ambayo wanadamu wanadhani ni ya muhimu.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Lakini Yesu akageuka, akamwambia Petro, “Ondoka mbele yangu Shetani! Wewe ni kikwazo kwangu. Mawazo yako si ya mungu bali ni ya kibinadamu!”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini Yesu akageuka, akamwambia Petro, “Ondoka mbele yangu, Shetani! Wewe ni kikwazo kwangu. Mawazo yako si ya kimungu ila ni ya kibinadamu!”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini Yesu akageuka na kumwambia Petro, “Rudi nyuma yangu, Shetani! Wewe ni kikwazo kwangu. Moyo wako hauwazi yaliyo ya Mungu, bali ya wanadamu.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini Isa akageuka na kumwambia Petro, “Rudi nyuma yangu, Shetani! Wewe ni kikwazo kwangu. Moyo wako hauwazi yaliyo ya Mungu, bali ya wanadamu.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akageuka, akamwambia Petro, Nenda nyuma yangu, Shetani; u kikwazo kwangu; maana huyawazi yaliyo ya Mungu, bali ya wanadamu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini Yesu akageuka, akamwambia Petro, “Ondoka mbele yangu, Shetani! Wewe ni kikwazo kwangu. Mawazo yako si ya kimungu ila ni ya kibinadamu!”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye akageuka, akamwambia Petero: Niondokea hapa nyuma yangu, wewe Satani! Wewe wataka kunikwaza, kwani wewe huyawazi mambo ya Kimungu, ila unayawaza ya kiwatu tu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akageuka, akamwambia Petro, Nenda nyuma yangu, Shetani; u kikwazo kwangu; maana huyawazi yaliyo ya Mungu, bali ya wanadamu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini Yesu akageuka na kumwambia: “Ondoka hapa karibu nami, wewe Shetani! Wewe ni kikwazo kwangu, kwa maana mawazo yako si ya Mungu, lakini ni ya kimutu.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Akageuka, akamwambia Petro, Nenda nyuma yangu, Shetani; u chukizo kwangu: maana huyawazi mambo ya Mungu, bali yaliyo ya wana Adamu.