Matthew 16:26 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
lakini mtu anayeyapoteza maisha yake kwa ajili yangu, atayapata. Je, mtu atafaidi nini akiupata utajiri wote wa ulimwengu na hali amepoteza maisha yake? Au, mtu atatoa kitu gani kiwe badala ya maisha yake?
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa maana itamfaidi mtu nini kuupata ulimwengu wote, lakini akayapoteza maisha yake? Au mtu atatoa nini badala ya nafsi yake?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwani atafaidiwa nini mtu akiupata ulimwengu wote, na kupata hasara ya nafsi yake? Au mtu atatoa nini badala ya nafsi yake?
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Haina maana kwenu ninyi kuupata ulimwengu wote, ikiwa ninyi wenyewe mtapotea. Mtu atalipa nini ili kuyapata tena maisha yake baada ya kuyapoteza?
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
lakini mtu anayeyapoteza maisha yake kwa ajili yangu, atayapata. Je, mtu atafaidi nini akiupata utajiri wote wa ulimwengu na hali amepoteza maisha yake? Au, mtu atatoa kitu gani kiwe badala ya maisha yake?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
lakini mtu anayeyapoteza maisha yake kwa ajili yangu, atayapata. Je, mtu atafaidi nini akiupata utajiri wote wa ulimwengu na hali amepoteza maisha yake? Au, mtu atatoa kitu gani kiwe badala ya maisha yake?
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa maana itamfaidia nini mtu kuupata ulimwengu wote, lakini akayapoteza maisha yake? Au mtu atatoa nini badala ya maisha yake?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa maana, je, itamfaidi nini mtu kuupata ulimwengu wote, lakini akayapoteza maisha yake? Au mtu atatoa nini badala ya nafsi yake?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwani atafaidiwa nini mtu akiupata ulimwengu wote, na kuipoteza nafsi yake? Au mtu atatoa nini badala ya nafsi yake?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
lakini mtu anayeyapoteza maisha yake kwa ajili yangu, atayapata. Je, mtu atafaidi nini akiupata utajiri wote wa ulimwengu na hali amepoteza maisha yake? Au, mtu atatoa kitu gani kiwe badala ya maisha yake?
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani mtu vitamfaa nini, hata avichume vya ulimwengu wote, roho yake ikiponwa navyo? Au mtu atatoa nini, aikomboe roho yake?*
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwani atafaidiwa nini mtu akiupata ulimwengu wote, na kupata hasara ya nafsi yake? Au mtu atatoa nini badala ya nafsi yake?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ni faida gani kwa mutu kupata utajiri wote wa dunia, lakini anapoteza uzima wake? Hakuna kitu mutu anachoweza kutoa kwa kukomboa uzima wake.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kwa maana atafaidiwa mtu nini akiupata ulimwengu wote, na kupata khasara ya roho yake? au mtu atatoa nini badala ya roho yake?