Matthew 16:4 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kizazi kiovu kisicho na uaminifu! Kinataka ishara, lakini hakitapewa ishara yoyote isipokuwa ishara ile ya Yona.” Basi, akawaacha, akaenda zake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kizazi kiovu na cha uzinzi kinatafuta ishara, lakini hakitapewa ishara yoyote isipokuwa ishara ya Yona.” Isa akawaacha, akaenda zake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kizazi kibaya na cha zinaa chataka ishara; wala hakitapewa ishara, isipokuwa ishara ya Yona. Akawaacha, akaenda zake.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ninyi watu mnaoishi sasa ni waovu na si waaminifu kwa Mungu. Ndiyo sababu kabla ya kuamini mnataka kuona muujiza. Lakini hakuna muujiza utakaofanyika ili kuwathibitishia kitu cho chote. Yona ndiyo ishara pekee mtakayopewa.” Kisha Yesu akaondoka mahali pale.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kizazi kiovu kisicho na uaminifu! Mnataka ishara, lakini hamtapewa ishara yoyote isipokuwa tu ile ya Yona.” Basi, akawaacha, akaenda zake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kizazi kiovu kisicho na uaminifu! Kinataka ishara, lakini hakitapewa ishara yoyote isipokuwa ishara ile ya Yona.” Basi, akawaacha, akaenda zake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kizazi cha waovu na cha zinaa hutafuta ishara ya majira, lakini hakitapewa ishara yo yote isipokuwa ishara ya Yona.” Yesu akawaacha, akaenda zake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kizazi kiovu na cha uzinzi kinatafuta ishara, lakini hakitapewa ishara yoyote isipokuwa ishara ya Yona.” Isa akawaacha, akaenda zake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kizazi kibaya na cha zinaa chataka ishara; wala hakitapewa ishara, isipokuwa ishara ya Yona. Akawaacha, akaenda zake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kizazi kiovu kisicho na uaminifu! Kinataka ishara, lakini hakitapewa ishara yoyote isipokuwa ishara ile ya Yona.” Basi, akawaacha, akaenda zake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wao wa ukoo huu mbaya wenye ugoni wanataka kielekezo, lakini hawatapata kielekezo, ila kielekezo cha mfumbuaji Yona. Kisha akawaacha, akaenda zake.*
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kizazi kibaya na cha zinaa chataka ishara; wala hakitapewa ishara, isipokuwa ishara ya Yona. Akawaacha, akaenda zake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Watu wa kizazi kibaya na kinachokosa uaminifu mbele ya Mungu wanataka kuona kitambulisho. Lakini hawataonyeshwa kitambulisho isipokuwa kitambulisho cha nabii Yona.” Kisha Yesu akawaacha na kujiendea.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kizazi kibaya na cha zina chataka ishara; wala hakitapewa ishara, isipokuwa ishara ya nabii Yunus. Akawaacha, akaenda zake.