Matthew 17:2 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Huko, Yesu akageuka sura mbele yao, uso wake ukangaa kama jua na mavazi yake yakawa meupe kama mwanga.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wakiwa huko, Isa alibadilika sura mbele yao. Uso wake ukang’aa kama jua na nguo zake zikawa nyeupe kama nuru.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
akageuka sura yake mbele yao; uso wake ukang'aa kama jua, mavazi yake yakawa meupe kama nuru.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Wafuasi wake hawa walipokuwa wakimwangalia, Yesu alibadilika. Uso wake ukawa angavu kama jua na nguo zake zikawa nyeupe kama mwanga.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Huko, wakiwa wanamtazama, akageuka sura, uso wake ukang'aa kama jua na mavazi yake yakawa meupe kama nuru.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Huko, Yesu akageuka sura mbele yao, uso wake ukang'aa kama jua na mavazi yake yakawa meupe kama mwanga.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakiwa huko, Yesu alibadilika sura mbele yao. Uso wake ukang'aa kama jua na nguo zake zikawa na weupe wa kuumiza macho.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakiwa huko, Isa alibadilika sura mbele yao. Uso wake ukang’aa kama jua na nguo zake zikawa na weupe wa kuumiza macho.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
akageuka sura yake mbele yao; uso wake ukang'aa kama jua, mavazi yake yakawa meupe kama nuru.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Huko, Yesu akageuka sura mbele yao, uso wake ukangaa kama jua na mavazi yake yakawa meupe kama mwanga.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Huko akageuzwa sura yake machoni pao. Uso wake ukamulika kama jua, nazo nguo zake zikamerimeta kama mwanga.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
akageuka sura yake mbele yao; uso wake ukang’aa kama jua, mavazi yake yakawa meupe kama nuru.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na kule sura ya Yesu ikageuka wazi mbele yao. Uso wake ukangaa kama jua, nazo nguo zake zikametameta kama mwangaza.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
akageuka sura yake mbele yao: uso wake ukangʼaa kama jua, mavazi yake yakawa meupe kama nuru.