Matthew 17:26 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Petro akajibu, “Kutoka kwa wageni.” Yesu akamwambia, “Haya basi, wananchi hawahusiki.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Petro akamjibu, “Kutoka kwa watu wengine.” Isa akamwambia, “Kwa hiyo watoto wao wamesamehewa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye aliposema, Kwa wageni, Yesu alimwambia, Basi, kama ni hivyo, wana ni mahuru.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Petro akajibu, “Watu wengine ndiyo hulipa kodi.” Yesu akasema, “Basi wana wa mfalme hawapaswi kulipa kodi.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Petro akajibu, “Kutoka kwa wageni.” Yesu akamwambia, “Haya basi, wananchi hawahusiki.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Petro akajibu, “Kutoka kwa wageni.” Yesu akamwambia, “Haya basi, wananchi hawahusiki.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Petro akamjibu, “Kutoka kwa watu wengine.” Yesu akamwambia, “Kwa hiyo watoto wao wamesamehewa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Petro akamjibu, “Kutoka kwa watu wengine.” Isa akamwambia, “Kwa hiyo watoto wao wamesamehewa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye aliposema, Kwa wageni, Yesu alimwambia, Basi, kama ni hivyo, wana wako huru.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Petro akajibu, “Kutoka kwa wageni.” Yesu akamwambia, “Haya basi, wananchi hawahusiki.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Alipojibu: Huwatoza wageni, Yesu akamwambia: Basi, wana wenyewe hawatozwi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye aliposema, Kwa wageni, Yesu alimwambia, Basi, kama ni hivyo, wana ni mahuru.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Petro akamujibu: “Watu wengine.” Na Yesu akamwambia: “Basi ni kusema kwamba watu wa jamaa zao wako na ruhusa ya kutolipa.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Petro akamwambia, Kwa wageni. Yesu akamwambia, Bassi, kama ni hivyo, wana ni huru.