Matthew 17:5 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Alipokuwa bado anasema hivyo, wingu jeupe likawafunika, na sauti ikasikika kutoka hilo wingu: “Huyu ni Mwanangu mpendwa, ninayependezwa naye, msikilizeni.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Petro alipokuwa angali ananena, ghafula wingu lililong’aa likawafunika, na sauti ikatoka kwenye hilo wingu ikisema, “Huyu ni Mwanangu mpendwa. Ninapendezwa naye sana. Msikieni yeye.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Alipokuwa katika kusema, tazama, wingu jeupe likawatia uvuli; na tazama, sauti ikatoka katika lile wingu, ikasema, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye; msikieni yeye.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Petro alipokuwa akizungumza, wingu jeupe liliwafunika. Sauti ikatoka katika wingu na akasema, “Huyu ni Mwanangu, ninayempenda, ninafurahishwa naye. Mtiini yeye!”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Alipokuwa bado anasema hivyo, wingu jeupe likawafunika, na sauti ikasikika kutoka katika hilo wingu: “Huyu ni Mwanangu mpendwa, ninayependezwa naye, msikilizeni.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Alipokuwa bado anasema hivyo, wingu jeupe likawafunika, na sauti ikasikika kutoka hilo wingu: “Huyu ni Mwanangu mpendwa, ninayependezwa naye, msikilizeni.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Petro alipokuwa angali ananena, ghafula, wingu linalong'aa likawafunika na sauti ikatoka kwenye hilo wingu ikisema, “Huyu ni mwanangu mpendwa, ninayependezwa naye sana, msikilizeni yeye.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Petro alipokuwa angali ananena, ghafula wingu lililong’aa likawafunika, na sauti ikatoka kwenye hilo wingu ikisema, “Huyu ni Mwanangu mpendwa. Ninapendezwa naye sana. Msikieni yeye.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Alipokuwa bado akisema, tazama, wingu jeupe likawatia uvuli; na tazama, sauti ikatoka katika lile wingu, ikasema, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye; msikieni yeye.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Alipokuwa bado anasema hivyo, wingu jeupe likawafunika, na sauti ikasikika kutoka hilo wingu: “Huyu ni Mwanangu mpendwa, ninayependezwa naye, msikilizeni.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Angali akisema, mara wingu jeupe likawatia kivuli, sauti ikatoka winguni, ikisema: Huyu ndiye mwanangu mpendwa, ambaye nimependezwa naye. Msikilizeni yeye!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Alipokuwa katika kusema, tazama, wingu jeupe likawatia uvuli; na tazama, sauti ikatoka katika lile wingu, ikasema, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye; msikieni yeye.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Naye alipokuwa angali akisema, wingu lenye kuangaza likawafunika, na sauti ikasikilika toka katikati ya lile wingu ikisema: “Huyu ni Mwana wangu mupendwa, ninapendezwa naye sana. Mumusikilize!”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Alipokuwa akisema, wingu jeupe likawatia uvuli; sauti ikatoka katika lile wingu, ikinena, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, niliyependezwa nae; msikieni yeye.