Matthew 17:6 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wanafunzi waliposikia hivyo wakaanguka kifudifudi, wakaogopa sana.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wanafunzi waliposikia haya, wakaanguka kifudifudi, wakajawa na hofu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na wale wanafunzi waliposikia, walianguka kifulifuli, wakaogopa sana.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Wafuasi waliokuwa na Yesu walipoisikia sauti hii waliogopa sana na wakaanguka chini.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Wanafunzi waliposikia hivyo wakaanguka kifudifudi, wakaogopa sana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wanafunzi waliposikia hivyo wakaanguka kifudifudi, wakaogopa sana.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wale wanafunzi, waliposikia haya, wakaanguka chini kifudifudi, wakajawa na hofu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wanafunzi waliposikia haya, wakaanguka chini kifudifudi, wakajawa na hofu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na wale wanafunzi waliposikia, walianguka kifudifudi na kuogopa sana.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wanafunzi waliposikia hivyo wakaanguka kifudifudi, wakaogopa sana.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wanafunzi walipoyasikia wakaanguka kifudifudi, wakaingiwa na woga sana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na wale wanafunzi waliposikia, walianguka kifulifuli, wakaogopa sana.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wanafunzi wale waliposikia sauti ile, wakaogopa sana, wakaanguka uso mpaka chini.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na wale wanafunzi waliposikia, wakaanguka kifudifudi, wakaogopa sana.