Matthew 18:12 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mnaonaje? Mtu akiwa na kondoo 100, akimpoteza mmoja, hufanyaje? Huwaacha wale tisini na tisa mlimani, akaenda kumtafuta yule aliyepotea.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Mwaonaje? Ikiwa mtu ana kondoo mia moja, na mmoja wao akapotea, je, hatawaacha wale tisini na tisa vilimani na kwenda kumtafuta huyo mmoja aliyepotea?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mwaonaje? Mtu akiwa na kondoo mia, mmoja akampotea, je! Hawaachi wale tisa na tisini, akaenda milimani, na kumtafuta yule aliyepotea?
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mtu akiwa na kondoo 100, lakini mmoja wa kondoo akapotea, atafanya nini? Atawaacha kondoo wengine 99 kwenye kilima na kwenda kumtafuta mmoja aliyepotea. Sawa?
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Mnaonaje? Mtu akiwa na kondoo mia, akimpoteza mmoja, hufanyaje? Huwaacha wale tisini na tisa mlimani, na huenda kumtafuta yule aliyepotea.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mnaonaje? Mtu akiwa na kondoo 100, akimpoteza mmoja, hufanyaje? Huwaacha wale tisini na tisa mlimani, akaenda kumtafuta yule aliyepotea.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Mwaonaje? Ikiwa mtu anao kondoo mia moja na mmoja wao akapotea, hatawaacha wale tisini na tisa vilimani na kwenda kumtafuta huyo mmoja aliyepotea?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Mwaonaje? Ikiwa mtu ana kondoo mia moja, na mmoja wao akapotea, je, hatawaacha wale tisini na tisa vilimani na kwenda kumtafuta huyo mmoja aliyepotea?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mwaonaje? Mtu akiwa na kondoo mia, mmoja akampotea, je! Hawaachi wale tisini na tisa, akaenda milimani, na kumtafuta yule aliyepotea?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mnaonaje? Mtu akiwa na kondoo 100, akimpoteza mmoja, hufanyaje? Huwaacha wale tisini na tisa mlimani, akaenda kumtafuta yule aliyepotea.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mwaonaje? Mtu akiwa na kondoo mia, tena mmoja wao akipotea, hatawaacha wale tisini na tisa milimani, aende kumtafuta yule aliyepotea?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mwaonaje? Mtu akiwa na kondoo mia, mmoja akampotea, je! Hawaachi wale tisa na tisini, akaenda milimani, na kumtafuta yule aliyepotea?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Munafikiri nini? Kama mutu akiwa na kondoo mia moja, na mumoja wao akipotea, hatawaacha wale wengine makumi tisa na tisa juu ya mulima na kwenda kumutafuta yule aliyepotea?
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Mwaonaje? mtu akiwa na kondoo mia, mmoja akampotea, je, hawaachi wale tissa na tissaini, akaenda milimani, na kumtafuta yule aliyepotea?