Matthew 18:15 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Ndugu yako akikukosea, mwendee ukamwonye mkiwa nyinyi peke yenu. Akikusikia utakuwa umempata ndugu yako.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Ndugu yako akikukosea, nenda ukamwoneshe kosa lake, kati yenu ninyi wawili peke yenu. Akikusikiliza, utakuwa umempata tena ndugu yako.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na ndugu yako akikukosa, enenda ukamwonye, wewe na yeye peke yenu; akikusikia, umempata nduguyo.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ikiwa mmoja wa ndugu au dada yako katika familia ya Mungu akifanya kosa kwako, umwendee na umwambie kile alichokukosea. Ufanye hivi mnapokuwa ninyi wawili tu. Ikiwa mtu huyo atakusikiliza, basi umemsaidia na umfanye kuwa kaka ama dada yako tena.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
“Ndugu yako akikukosea, mwendee ukamwonye mkiwa ninyi peke yenu. Akikusikia utakuwa umempata ndugu yako.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Ndugu yako akikukosea, mwendee ukamwonye mkiwa nyinyi peke yenu. Akikusikia utakuwa umempata ndugu yako.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Kama ndugu yako akikukosea, nenda ukamwonyeshe kosa lake, kati yenu ninyi wawili peke yenu. Kama akikusikiliza, utakuwa umempata tena ndugu yako.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Kama ndugu yako akikukosea, nenda ukamwonyeshe kosa lake, kati yenu ninyi wawili peke yenu. Kama akikusikiliza, utakuwa umempata tena ndugu yako.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na ndugu yako akikukosea, nenda ukamwonye, wewe na yeye peke yenu; akikusikia, umempata nduguyo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Ndugu yako akikukosea, mwendee ukamwonye mkiwa nyinyi peke yenu. Akikusikia utakuwa umempata ndugu yako.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndugu yako akikukosea, nenda kamwonye, wewe na yeye mko peke yenu! Akikusikia, umempata tena ndugu yako.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na ndugu yako akikukosa, enenda ukamwonye, wewe na yeye peke yenu; akikusikia, umempata nduguyo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Kama ndugu yako akikukosea, umwendee kwa kumwonyesha kosa lake, mukiwa ninyi wawili peke yenu. Na kama akikusikia, unarudiliana na ndugu yako.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na ndugu yako akikutenda dhambi, enenda ukamwonye, wewe na yeye peke yenu: akikusikia, umempata ndugu yako.