Matthew 18:16 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Asipokusikia, chukua mtu mmoja au wawili pamoja nawe, ili kwa mawaidha ya mashahidi wawili au watatu, kila tatizo litatuliwe.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini asipokusikiliza, nenda na mtu mwingine mmoja au wawili ili kila neno ‘lithibitishwe kwa ushahidi wa mashahidi wawili au watatu’.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
La, kama hasikii, chukua pamoja nawe tena mtu mmoja au wawili, ili kwa vinywa vya mashahidi wawili au watatu kila neno lithibitike.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Lakini ikiwa mtu huyo atakataa kukusikiliza, mrudie ukiwa pamoja na ndugu wengine wawili waaminio. Ndipo watakuwepo watu wawili au watatu watakaoweza kueleza kile kilichotokea.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Asipokusikia, chukua mtu mmoja au wawili pamoja nawe, ili kwa mawaidha ya mashahidi wawili au watatu, kila tatizo litatuliwe.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Asipokusikia, chukua mtu mmoja au wawili pamoja nawe, ili kwa mawaidha ya mashahidi wawili au watatu, kila tatizo litatuliwe.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini kama hatakusikiliza, nenda na mtu mwingine mmoja au wawili ili kila neno lithibitishwe na ushahidi wa mashahidi wawili au watatu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini kama hatakusikiliza, nenda na mtu mwingine mmoja au wawili ili kila neno lithibitishwe kwa ushahidi wa mashahidi wawili au watatu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
La, kama hasikii, chukua pamoja nawe tena mtu mmoja au wawili, ili kwa vinywa vya mashahidi wawili au watatu kila neno lithibitike.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Asipokusikia, chukua mtu mmoja au wawili pamoja nawe, ili kwa mawaidha ya mashahidi wawili au watatu, kila tatizo litatuliwe.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini asipokusikia, chukua pamoja na wewe tena mmoja au wawili! Maana kila shauri limalizike kwa kusemewa na mashahidi wawili au watatu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
La, kama hasikii, chukua pamoja nawe tena mtu mmoja au wawili, ili kwa vinywa vya mashahidi wawili au watatu kila neno lithibitike.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini kama akikataa kukusikia, utwae mutu mumoja au wawili na kumwendea pamoja nao, kusudi kila neno lihakikishwe kwa ushuhuda wa watu wawili au watatu, sawa vile Maandiko Matakatifu yanavyosema.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
La, hakusikia, chukua pamoja nawe tena mtu mmoja au wawili, illi kwa vinywa vya mashahidi wawili au watatu killa neno lithubutike.