Matthew 18:17 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Asipowasikia hao, liambie kanisa. Na kama hatalisikia kanisa, na awe kwako kama watu wasiomjua Mungu na watozaushuru.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akikataa kuwasikiliza hao, waambieni kundi lenu la waumini. Naye akikataa hata kuwasikiliza kundi la waumini, basi awe kwenu kama mtu asiyeamini au mtoza ushuru.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na asipowasikiliza wao, liambie kanisa; na asipolisikiliza kanisa pia, na awe kwako kama mtu wa mataifa na mtoza ushuru.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ikiwa mtu aliyetenda dhambi atakataa kuwasikiliza, ndipo uliambie kanisa. Na akikataa kulisikiliza kanisa, mchukulie kama ambavyo ungemchukulia mtu asiyemfahamu Mungu au mtoza ushuru.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Asipowasikia hao, liambie kanisa. Na kama hatalisikia kanisa, na awe kwako kama watu wasiomjua Mungu na watoza ushuru.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Asipowasikia hao, liambie kanisa. Na kama hatalisikia kanisa, na awe kwako kama watu wasiomjua Mungu na watozaushuru.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kama akikataa kuwasikiliza hao, liambie kanisa, naye kama akikataa hata kulisikiliza kanisa, basi mtendeeni mtu huyo kama vile ambavyo mngemtendea asiyeamini.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kama akikataa kuwasikiliza hao, ambieni kundi lenu la waumini. Naye kama akikataa hata kulisikiliza kundi la waumini, basi awe kwenu kama mtu asiyeamini au mtoza ushuru.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na asipowasikiliza wao, liambie kanisa; na asipolisikiliza kanisa pia, na awe kwako kama mtu wa mataifa na mtoza ushuru.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Asipowasikia hao, liambie kanisa. Na kama hatalisikia kanisa, na awe kwako kama watu wasiomjua Mungu na watozaushuru.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye akikataa kuwasikia hao, waambie wateule wenziwe shauri hilo! Lakini atakapokataa kuwasikia nao wateule, awe kwako kama mtu wa kimizimu au mtoza kodi!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na asipowasikiliza wao, liambie kanisa; na asipolisikiliza kanisa pia, na awe kwako kama mtu wa mataifa na mtoza ushuru.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na kama akikataa kuwasikia watu wale, upeleke habari kwa kanisa. Naye akikataa kusikia kanisa vilevile, umuhesabu kama mupagani na mutenda maovu sawa walipishaji wa kodi.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na asipowasikiliza wao, liambie kanisa: na asipolisikiliza kanisa pia, na awe sawasawa na mtu wa Mataifa na mtoza ushuru.