Matthew 18:19 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Tena nawaambieni, wawili miongoni mwenu wakikubaliana hapa duniani kuhusu jambo lolote la kuomba, Baba yangu wa mbinguni atawafanyia jambo hilo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Tena nawaambia, ikiwa wawili wenu watakubaliana duniani kuhusu jambo lolote watakaloomba, watatendewa na Baba yangu aliye mbinguni.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena nawaambia, ya kwamba wawili wenu watakapopatana duniani katika jambo lo lote watakaloliomba, watafanyiwa na Baba yangu aliye mbinguni.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kwa namna nyingine, ikiwa watu wawili waliopo duniani watakubaliana kwa kila wanachokiombea, Baba yangu wa mbinguni atatenda kile wanachokiomba.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Tena nawaambieni, wawili miongoni mwenu wakikubaliana hapa duniani kuhusu jambo lolote la kuomba, Baba yangu wa mbinguni atawafanyia jambo hilo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Tena nawaambieni, wawili miongoni mwenu wakikubaliana hapa duniani kuhusu jambo lolote la kuomba, Baba yangu wa mbinguni atawafanyia jambo hilo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Tena nawaambia, ikiwa wawili wenu watakubaliana duniani kuhusu jambo lo lote watakaloomba, watafanyiwa na Baba yangu aliye mbinguni.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Tena nawaambia, ikiwa wawili wenu watakubaliana duniani kuhusu jambo lolote watakaloomba, watafanyiwa na Baba yangu aliye mbinguni.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena nawaambia, ya kwamba wawili wenu watakapopatana duniani katika jambo lolote watakaloliomba, watafanyiwa na Baba yangu aliye mbinguni.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Tena nawaambieni, wawili miongoni mwenu wakikubaliana hapa duniani kuhusu jambo lolote la kuomba, Baba yangu wa mbinguni atawafanyia jambo hilo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tena nawaambiani: Kila jambo, wenzenu wawili nchini watakalopatana kuliomba, watapewa na Baba yangu alioko mbinguni.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena nawaambia, ya kwamba wawili wenu watakapopatana duniani katika jambo lo lote watakaloliomba, watafanyiwa na Baba yangu aliye mbinguni.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Kweli ninawaambia tena: wawili kati yenu hapa katika dunia wakipatana kwa kuomba juu ya kitu chochote, Baba yangu anayekuwa mbinguni atawapa kitu kile.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Tena nawaambieni, ya kwamba wawili wenu watakapopatana duniani katika jambo lo lote watakaloliomba, watafanyiwa na Baba yangu aliye mbinguni.