Matthew 18:24 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ukaguzi ulipoanza, akaletewa mtu mmoja aliyekuwa na deni la fedha talanta 10,000.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Alipoanza kufanya hesabu zake, mtu mmoja aliyekuwa anadaiwa talanta elfu kumi aliletwa kwake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Alipoanza kuifanya, aliletewa mtu mmoja awiwaye talanta
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mtumishi aliyekuwa anadaiwa na mfalme tani 300 za fedha aliletwa kwake.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Ukaguzi ulipoanza, akaletewa mtu mmoja aliyekuwa na deni la fedha talanta elfu kumi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ukaguzi ulipoanza, akaletewa mtu mmoja aliyekuwa na deni la fedha talanta 10,000.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Alipoanza kufanya hesabu zake, mtu mmoja aliyekuwa anadaiwa talanta 10,000, aliletwa kwake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Alipoanza kufanya hesabu zake, mtu mmoja aliyekuwa anadaiwa talanta 10,000, aliletwa kwake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Alipoanza kuifanya, aliletewa mtu mmoja mwenye deni la talanta elfu kumi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ukaguzi ulipoanza, akaletewa mtu mmoja aliyekuwa na deni la fedha talanta 10,000.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Alipoanza kuhesabu akaletewa mmoja mwenye madeni ya mizigo 10000 ya fedha.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Alipoanza kuifanya, aliletewa mtu mmoja awiwaye talanta elfu kumi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Alipoanza kufanya hesabu ile, wakamuletea mutumishi mumoja aliyekuwa na deni lake la mamilioni ya feza.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Alipoanza kuifanya, akaletewa mtu mmoja awiwae nae talanta elfu kumi.