Matthew 18:28 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Lakini huyo mtumishi akaondoka, akamkuta mmoja wa watumishi wenzake aliyekuwa na deni lake fedha dinari 100. Akamkamata, akamkaba koo akisema, ‘Lipa deni lako!’
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Lakini yule mtumishi alipokuwa anatoka nje, akakutana na mtumishi mwenzake aliyekuwa amemkopesha dinari mia moja. Akamkamata, akamkaba koo akimwambia, ‘Nilipe kile ninachokudai!’
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mtumwa yule akatoka, akamwona mmoja wa wajoli wake, aliyemwia dinari
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Lakini mtumishi huyo alipoondoka, alimwona mtumishi mwingine aliyekuwa anamdai sarafu mia za fedha. Akamkaba shingo yake na akasema, ‘Nilipe pesa ninayokudai!’
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
“Lakini huyo mtumishi akaondoka, akamkuta mmoja wa watumishi wenzake aliyekuwa na deni lake fedha denari mia moja. Akamkamata, akamkaba koo akisema, Lipa deni lako!
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Lakini huyo mtumishi akaondoka, akamkuta mmoja wa watumishi wenzake aliyekuwa na deni lake fedha dinari 100. Akamkamata, akamkaba koo akisema, ‘Lipa deni lako!’
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Lakini yule mtumishi alipokuwa anatoka nje, akakutana na mtumishi mwenzake aliyekuwa amemkopesha dinari mia moja. Akamkamata, akamkaba koo akimwambia, ‘Nilipe kile ninachokudai!’
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Lakini yule mtumishi alipokuwa anatoka nje, akakutana na mtumishi mwenzake aliyekuwa amemkopesha dinari mia moja. Akamkamata, akamkaba koo akimwambia, ‘Nilipe kile ninachokudai!’
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mtumwa yule akatoka, akamwona mmoja wa watumishi wake, aliyemwia dinari mia; akamkamata, akamkaba koo, akisema, Nilipe unachodaiwa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Lakini huyo mtumishi akaondoka, akamkuta mmoja wa watumishi wenzake aliyekuwa na deni lake fedha dinari 100. Akamkamata, akamkaba koo akisema, ‘Lipa deni lako!’
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini yule mtumwa alipotoka akamwona mtumwa mwenziwe mmoja aliyekuwa mdeni wake wa shilingi 100. Akamkamata, akamshika koo, akasema: Lipa deni lako!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mtumwa yule akatoka, akamwona mmoja wa wajoli wake, aliyemwia dinari mia; akamkamata, akamshika koo, akisema, Nilipe uwiwacho.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Mutumishi yule alipoondoka, akakutana na mumoja wa watumishi wenzake aliyekuwa na deni lake la vikoroti mia moja vya feza. Akamukamata na kumunyonganyonga shingo na kumulazimisha kulipa deni lake.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Mtumishi yule akatoka, akamwona mmoja wa wajoli wake, aliyewiwa nae dinari mia; akamkamata, akamshika koo, akinena, Nilipe uwiwacho.