Matthew 18:31 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Basi, watumishi wenzake walipoona jambo hilo walisikitika sana, wakaenda kumpasha habari bwana wao juu ya mambo hayo yaliyotukia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Watumishi wenzake walipoona haya yaliyotukia wakaudhika sana, nao wakaenda na kumwambia bwana wao kila kitu kilichokuwa kimetukia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi wajoli wake walipoyaona yaliyotendeka, walisikitika sana, wakaenda wakamweleza bwana wao yote yaliyotendeka.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Watumishi wengine walipoona hili, walimhurumia mtumishi aliyefungwa gerezani. Hivyo walienda na kumwambia mfalme kila kitu kilichotokea.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
“Basi, watumishi wenzake walipoona jambo hilo walisikitika sana, wakaenda kumpasha habari bwana wao juu ya mambo hayo yaliyotukia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Basi, watumishi wenzake walipoona jambo hilo walisikitika sana, wakaenda kumpasha habari bwana wao juu ya mambo hayo yaliyotukia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Watumishi wenzake walipoona haya yaliyotukia wakaudhika sana, nao wakaenda na kumwambia bwana wao kila kitu kilichokuwa kimetukia.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Watumishi wenzake walipoona haya yaliyotukia wakaudhika sana, nao wakaenda na kumwambia bwana wao kila kitu kilichokuwa kimetukia.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi watumwa wenzake walipoyaona yaliyotendeka, walisikitika sana, wakaenda wakamweleza bwana wao yote yaliyotendeka.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Basi, watumishi wenzake walipoona jambo hilo walisikitika sana, wakaenda kumpasha habari bwana wao juu ya mambo hayo yaliyotukia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Basi, watumwa wenziwe walipoyaona yaliyokuwa wakasikitika sana. Wakaja, wakamweleza bwana wao hayo yote yaliyokuwa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi wajoli wake walipoyaona yaliyotendeka, walisikitika sana, wakaenda wakamweleza bwana wao yote yaliyotendeka.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nao watumishi wenzake walipoona jambo hilo, wakahuzunika sana, wakaenda kumwelezea bwana wao yote yaliyotokea.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Bassi wajoli wake walipoyaona yaliyotendeka, wakasikitika sana, wakaenda wakamfafanulia bwana wao yote yaliyotendeka.