Matthew 18:6 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Yeyote atakayemkosesha mmoja wa hawa wadogo wanaoniamini, ingekuwa afadhali afungwe shingoni jiwe kubwa la kusagia na kuzamishwa kwenye kilindi cha bahari.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Lakini kama mtu yeyote akimsababisha mmoja wa hawa wadogo wanaoniamini kutenda dhambi, ingekuwa bora kwake afungiwe jiwe kubwa la kusagia shingoni mwake, na kutoswa katika kilindi cha bahari.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
bali atakayemkosesha mmojawapo wa wadogo hawa waniaminio, yamfaa afungiwe shingoni jiwe kubwa la kusagia, na kutoswa katika kilindi cha bahari.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ikiwa mmoja wa watoto hawa wadogo ananiamini, na mtu yeyote akasababisha mtoto huyo kutenda dhambi, ole wake mtu huyo. Ingekuwa bora mtu huyo kufungiwa jiwe la kusagia shingoni mwake na kuzamishwa katika kina kirefu baharini.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
“Yeyote atakayemkosesha mmoja wa hawa wadogo wanaoniamini, ingekuwa afadhali afungwe shingoni jiwe kubwa la kusagia na kuzamishwa kwenye kilindi cha bahari.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Yeyote atakayemkosesha mmoja wa hawa wadogo wanaoniamini, ingekuwa afadhali afungwe shingoni jiwe kubwa la kusagia na kuzamishwa kwenye kilindi cha bahari.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini kama mtu ye yote anamsababisha mmojawapo wa hawa wadogo wanaoniamini atende dhambi, ingekuwa bora kwake afungiwe jiwe kubwa la kusagia shingoni mwake na kutoswa katika kilindi cha bahari.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini kama mtu yeyote akimsababisha mmojawapo wa hawa wadogo wanaoniamini kutenda dhambi, ingekuwa bora kwake afungiwe jiwe kubwa la kusagia shingoni mwake, na kutoswa katika kilindi cha bahari.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
bali atakayemkosesha mmojawapo wa wadogo hawa waniaminio, yamfaa afungiwe shingoni jiwe kubwa la kusagia, na kutoswa katika kilindi cha bahari.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Yeyote atakayemkosesha mmoja wa hawa wadogo wanaoniamini, ingekuwa afadhali afungwe shingoni jiwe kubwa la kusagia na kuzamishwa kwenye kilindi cha bahari.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini mtu atakayekwaza mmoja tu aliye mwenzao hawa wadogo wanaonitegemea inamfaa kutungikwa shingoni pake jiwe kubwa la kusagia, kisha atoswe kilindini mwa bahari.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
bali atakayemkosesha mmojawapo wa wadogo hawa waniaminio, yamfaa afungiwe shingoni jiwe kubwa la kusagia, na kutoswa katika kilindi cha bahari.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Lakini anayeangusha mumoja wa hawa wadogo wanaoniamini, ingalikuwa heri afungiwe jiwe kubwa la kusagia katika shingo na kuzamishwa ndani ya bahari.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
bali atakaekosesha mmoja wa wadogo hawa waniaminio, yamfaa afungwe jiwe kubwa la kusagia shingoni mwake, na kutoswa katika kilindi cha bahari.