Matthew 18:9 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Na jicho lako likikukosesha, lingoe na kulitupa mbali nawe. Afadhali kwako kuingia katika uhai ukiwa chongo, kuliko kutupwa katika moto wa Jehanamu ukiwa na macho yako yote mawili.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nalo jicho lako likikusababisha kutenda dhambi, ling’oe, ulitupe mbali. Ni afadhali kwako kuingia katika uzima ukiwa na jicho moja, kuliko kuwa na macho mawili lakini ukatupwa katika moto wa Jehanamu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na jicho lako likikukosesha, ling'oe, ukalitupe mbali nawe; ni afadhali kuingia katika uzima una chongo, kuliko kuwa na macho mawili, na kutupwa katika jehanum ya moto.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Jicho lako likikufanya utende dhambi, ling'oe na ulitupe. Ni bora kwako kuwa na jicho moja tu na ukaupata uzima wa milele kuliko kuwa na macho mawili na ukatupwa katika moto wa Jehanamu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Na kama jicho lako likikukosesha, ling'oe na kulitupa mbali nawe. Ni afadhali kwako kuingia katika uzima ukiwa chongo, kuliko kutupwa katika moto wa Jehanamu ukiwa na macho yako yote mawili.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Na jicho lako likikukosesha, ling'oe na kulitupa mbali nawe. Afadhali kwako kuingia katika uhai ukiwa chongo, kuliko kutupwa katika moto wa Jehanamu ukiwa na macho yako yote mawili.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nalo jicho lako kama linakusababisha utende dhambi ling'oe, ulitupe mbali. Ni afadhali kwako kuingia katika uzima ukiwa na jicho moja, kuliko kuwa na macho mawili ukatupwa katika moto wa jehanamu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nalo jicho lako likikusababisha kutenda dhambi, ling’oe, ulitupe mbali. Ni afadhali kwako kuingia katika uzima ukiwa na jicho moja, kuliko kuwa na macho mawili lakini ukatupwa katika moto wa Jehanamu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na jicho lako likikukosesha, ling'oe, ukalitupe mbali nawe; ni afadhali kuingia katika uzima ukiwa na chongo, kuliko kuwa na macho mawili, na kutupwa katika Jehanamu ya moto.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Na jicho lako likikukosesha, lingoe na kulitupa mbali nawe. Afadhali kwako kuingia katika uhai ukiwa chongo, kuliko kutupwa katika moto wa Jehanamu ukiwa na macho yako yote mawili.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nalo jicho lako likikukwaza, basi ling'oe ulitupe mbali! Kuingia penye uzima mwenye chongo kutakufaa kuliko hapo, ukiwa mwenye macho mawili, ukatupwa shimoni mwa moto.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na jicho lako likikukosesha, ling’oe, ukalitupe mbali nawe; ni afadhali kuingia katika uzima una chongo, kuliko kuwa na macho mawili, na kutupwa katika jehanum ya moto.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na kama jicho lako likikukosesha, uliongoe na kulitupa mbali! Ni heri kwako kuingia pahali utakapopata uzima wa kweli ukikuwa na jicho moja kuliko kuwa na macho mawili na kutupwa katika moto wa jehenamu.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na jicho lako likikukosesha, lingʼoe, ukalitupe mbali nawe; ni vyema zaidi kuingia katika uzima una chongo, kuliko kuwa na macho mawili, na kutupwa katika jebannum ya moto.