Matthew 19:12 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Maana kuna sababu kadhaa za kutoweza kuoa: Wengine ni kwa sababu wamezaliwa hivyo, wengine kwa sababu wamefanywa hivyo na watu, na wengine wameamua kutooa kwa ajili ya ufalme wa mbinguni. Awezaye kulipokea fundisho hili na alipokee.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa maana wengine ni matowashi kwa sababu wamezaliwa hivyo; wengine wamefanywa matowashi na wanadamu; na wengine wamejifanya matowashi kwa ajili ya ufalme wa mbinguni. Yeye awezaye kulipokea neno hili na alipokee.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana wako matowashi waliozaliwa hali hiyo toka matumboni mwa mama zao; tena wako matowashi waliofanywa na watu kuwa matowashi; tena wako matowashi waliojifanya kuwa matowashi kwa ajili ya ufalme wa mbinguni. Awezaye kulipokea neno hili, na alipokee.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kuna sababu tofauti kwa nini baadhi ya wanaume hawaoi. Wengine wamezaliwa wakiwa hawana uwezo wa kuzaa watoto, wengine walifanywa hivyo katika maisha yao ya baadaye. Na wengine walichagua kutokuoa kwa ajili ya ufalme wa Mungu. Hili liko hivyo kwa kila anayeweza kulikubali.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Maana kuna sababu kadhaa za kutoweza kuoa: wengine ni kwa sababu wamezaliwa hivyo, wengine kwa sababu wamefanywa hivyo na watu, na wengine wameamua kutooa kwa ajili ya Ufalme wa mbinguni. Awezaye kulipokea fundisho hili na alipokee.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Maana kuna sababu kadhaa za kutoweza kuoa: wengine ni kwa sababu wamezaliwa hivyo, wengine kwa sababu wamefanywa hivyo na watu, na wengine wameamua kutooa kwa ajili ya ufalme wa mbinguni. Awezaye kulipokea fundisho hili na alipokee.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa maana wengine ni matowashi kwa sababu wamezaliwa hivyo, wengine wamefanywa matowashi na wanadamu, na wengine wamejifanya matowashi kwa ajili ya Ufalme wa Mbinguni. Yeye awezaye kulipokea neno hili na alipokee.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa maana wengine ni matowashi kwa sababu wamezaliwa hivyo; wengine wamefanywa matowashi na wanadamu; na wengine wamejifanya matowashi kwa ajili ya Ufalme wa Mbinguni. Yeye awezaye kulipokea neno hili na alipokee.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana wako matowashi waliozaliwa hali hiyo toka matumboni mwa mama zao; tena wako matowashi waliofanywa na watu kuwa matowashi; tena wako matowashi waliojifanya kuwa matowashi kwa ajili ya ufalme wa mbinguni. Awezaye kulipokea neno hili, na alipokee.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Maana kuna sababu kadhaa za kutoweza kuoa: Wengine ni kwa sababu wamezaliwa hivyo, wengine kwa sababu wamefanywa hivyo na watu, na wengine wameamua kutooa kwa ajili ya ufalme wa mbinguni. Awezaye kulipokea fundisho hili na alipokee.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani katika watu wasiozaa, wako waliozaliwa hivyo tangu tumboni mwa mama zao. Tena wako wengine waliokomeshwa na watu, wasizae. Tena wako wengine waliojikomesha wenyewe, wasizae kwa ajili ya ufalme wa mbingu. Anayeweza kuitambua maana na aitambue!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana wako matowashi waliozaliwa hali hiyo toka matumboni mwa mama zao; tena wako matowashi waliofanywa na watu kuwa matowashi; tena wako matowashi waliojifanya kuwa matowashi kwa ajili ya ufalme wa mbinguni. Awezaye kulipokea neno hili, na alipokee.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kulingana na hayo, watu wamoja hawawezi kuoa kwa sababu walizaliwa towashi, wengine wamefanywa kuwa towashi na watu, wengine wamejifanya vile wenyewe kwa sababu ya kutumikia Ufalme wa mbinguni. Anayeweza kukubali mafundisho haya, ayakubali!”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Maana wako matawashi waliozaliwa katika hali hii toka matumboni mwa mama zao; teua wako matawashi waliofanywa kuwa matawashi na watu: tena wako matawashi waliojifanya kuwa matawashi kwa ajili ya ufalme wa mbinguni. Awezae kulipokea neno hili, na alipokee.