Matthew 19:13 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha watu wakamletea Yesu watoto wadogo ili awawekee mikono na kuwaombea. Lakini wanafunzi wakawakemea.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha watoto wadogo wakaletwa kwa Isa ili aweke mikono yake juu yao na awaombee. Lakini wanafunzi wake wakawakemea wale waliowaleta.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo akaletewa watoto wadogo ili aweke mikono yake juu yao na kuwaombea; wanafunzi wake wakawakemea.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ndipo watu wakawaleta watoto wao wadogo kwa Yesu ili awabariki na kuwaombea. Wafuasi wake walipoliona hili, waliwakataza watu wasiwalete watoto kwa Yesu.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kisha watu wakamletea Yesu watoto wadogo ili awawekee mikono na kuwaombea. Lakini wanafunzi wakawakemea.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha watu wakamletea Yesu watoto wadogo ili awawekee mikono na kuwaombea. Lakini wanafunzi wakawakemea.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha watoto wadogo wakaletwa kwa Yesu ili aweke mikono yake juu yao na awaombee. Lakini wanafunzi wake wakawakemea wale waliowaleta.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha watoto wadogo wakaletwa kwa Isa ili aweke mikono yake juu yao na awaombee. Lakini wanafunzi wake wakawakemea wale waliowaleta.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndipo akaletewa watoto wadogo ili aweke mikono yake juu yao na kuwaombea; wanafunzi wake wakawakemea.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha watu wakamletea Yesu watoto wadogo ili awawekee mikono na kuwaombea. Lakini wanafunzi wakawakemea.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hapo ndipo, alipoletewa vitoto, awabandikie mikono na kuwaombea. Lakini wanafunzi waliwatisha.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo akaletewa watoto wadogo ili aweke mikono yake juu yao na kuwaombea; wanafunzi wake wakawakemea.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Watu wamoja walimuletea Yesu watoto kusudi awawekee mikono na kuwaombea, lakini wanafunzi wakawakaripia watu wale.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Ndipo akaletewa vitoto aweke mikono yake juu yao na kuwaombea; wanafunzi wake wakawakemea.