Matthew 19:17 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yesu akamwambia, “Mbona unaniuliza kuhusu jambo jema? Kuna mmoja tu aliye mwema. Ukitaka kuingia katika uhai, shika amri.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Isa akamjibu, “Mbona unaniuliza habari ya mema? Aliye mwema ni Mmoja tu. Lakini ukitaka kuingia uzimani, zitii amri.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akamwambia Kwani kuniuliza habari ya wema? Aliye mwema ni mmoja. Lakini ukitaka kuingia katika uzima, zishike amri.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Yesu akajibu, “Kwa nini unaniuliza kuhusu jambo gani lililo jema? Mungu pekee yake ndiye mwema. Lakini ikiwa unataka kuupata uzima wa milele, zitii amri.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Yesu akamwambia, “Mbona unaniuliza kuhusu jambo jema? Kuna mmoja tu aliye mwema. Ukitaka kuingia katika uzima, shika amri.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yesu akamwambia, “Mbona unaniuliza kuhusu jambo jema? Kuna mmoja tu aliye mwema. Ukitaka kuingia katika uhai, shika amri.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yesu akamjibu, “Mbona unaniita mimi mwema? Hakuna aliye mwema ila Mmoja tu, ndiye Mungu: Lakini ukitaka kuingia uzimani, zitii amri.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Isa akamjibu, “Mbona unaniuliza habari ya mema? Aliye mwema ni Mmoja tu. Lakini ukitaka kuingia uzimani, zitii amri.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akamwambia, Kwa nini uniulize kuhusu wema? Aliye mwema ni mmoja. Lakini ukitaka kuingia katika uzima, zishike amri.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yesu akamwambia, “Mbona unaniuliza kuhusu jambo jema? Kuna mmoja tu aliye mwema. Ukitaka kuingia katika uhai, shika amri.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye akamwambia: Unaniulizaje jambo lililo jema? Aliye mwema ni mmoja. Lakini ukitaka kuingia uzimani yashike maagizo!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akamwambia Kwani kuniuliza habari ya wema? Aliye mwema ni mmoja. Lakini ukitaka kuingia katika uzima, zishike amri.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yesu akamujibu: “Sababu gani unaniuliza juu ya jambo linalokuwa jema? Kuna mumoja tu anayekuwa mwema. Kama ukitaka kuingia pahali utakapopata uzima wa kweli, utii amri za Mungu.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Akamwambia, Ya nini kuniita mwema? Hakuna mwema illa mmoja, ndiye Mungu. Lakini ukitaka kuingia katika nzima, zishike amri.