Matthew 19:26 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yesu akawatazama, akasema, “Kwa binadamu jambo hili haliwezekani, lakini kwa Mungu mambo yote huwezekana.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini Isa akawatazama, akawaambia, “Kwa mwanadamu jambo hili haliwezekani, lakini mambo yote yanawezekana kwa Mungu.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Yesu akawakazia macho, akawaambia, Kwa wanadamu hilo haliwezekani; bali kwa Mungu yote yawezekana.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Yesu akawatazama na kuwaambia, “Hili haliwezekani kwa wanadamu, Lakini yote yanawezekana kwa Mungu.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Yesu akawatazama, akasema, “Kwa binadamu jambo hili haliwezekani, lakini kwa Mungu mambo yote huwezekana.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yesu akawatazama, akasema, “Kwa binadamu jambo hili haliwezekani, lakini kwa Mungu mambo yote huwezekana.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini Yesu akawatazama, akawaambia, “Kwa mwanadamu jambo hili haliwezekani, lakini kwa Mungu mambo yote yanawezekana.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini Isa akawatazama, akawaambia, “Kwa mwanadamu jambo hili haliwezekani, lakini mambo yote yanawezekana kwa Mungu.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Yesu akawakazia macho, akawaambia, Kwa wanadamu hilo haliwezekani; bali kwa Mungu yote yawezekana.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yesu akawatazama, akasema, “Kwa binadamu jambo hili haliwezekani, lakini kwa Mungu mambo yote huwezekana.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yesu akawachungua, akawaambia: Kwa watu neno hili haliwezekani, lakini kwa Mungu mambo yote huwezekana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Yesu akawakazia macho, akawaambia, Kwa wanadamu hilo haliwezekani; bali kwa Mungu yote yawezekana.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yesu akawaangalia na kuwaambia: “Jambo hilo haliwezi kutendeka kwa uwezo wa mwanadamu, lakini kwa uwezo wa Mungu, yote yanawezekana.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Yesu akawatazama, akawaambia, Kwa wana Adamu hili haliwezekani; bali kwa Mungu yote yawezekana.