Matthew 19:29 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Na kila aliyeacha nyumba, au ndugu, au dada, au baba, au mama, au watoto, au mashamba, kwa ajili yangu, atapokea mara mia zaidi, na kupata uhai wa milele.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kila mtu aliyeacha nyumba, au ndugu zake wa kiume au wa kike, baba au mama, watoto au mashamba kwa ajili yangu, atapokea mara mia zaidi ya hayo, na ataurithi uzima wa milele.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na kila mtu aliyeacha nyumba, au ndugu wa kiume au wa kike, au baba, au mama, au watoto, au mashamba, kwa ajili ya jina langu, atapokea mara mia, na kuurithi uzima wa milele.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kila aliyeacha nyumba, ndugu, dada, baba, mama, watoto au shamba na akanifuata atapata zaidi ya yale aliyoacha. Na atapata uzima wa milele.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Na kila aliyeacha nyumba, au ndugu, au dada, au baba, au mama, au watoto, au mashamba, kwa ajili yangu, atapokea mara mia zaidi, na kupata uzima wa milele.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Na kila aliyeacha nyumba, au ndugu, au dada, au baba, au mama, au watoto, au mashamba, kwa ajili yangu, atapokea mara mia zaidi, na kupata uhai wa milele.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kila mmoja aliyeacha nyumba au ndugu zake wa kiume au wa kike au baba au mama au watoto au mashamba kwa ajili yangu, atapokea mara mia zaidi ya hayo na ataurithi uzima wa milele.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kila mtu aliyeacha nyumba, au ndugu zake wa kiume au wa kike, baba au mama, watoto au mashamba kwa ajili yangu, atapokea mara mia zaidi ya hayo, na ataurithi uzima wa milele.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na kila mtu aliyeacha nyumba, au ndugu wa kiume au wa kike, au baba, au mama, au watoto, au mashamba, kwa ajili ya jina langu, atapokea mara mia, na kuurithi uzima wa milele.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Na kila aliyeacha nyumba, au ndugu, au dada, au baba, au mama, au watoto, au mashamba, kwa ajili yangu, atapokea mara mia zaidi, na kupata uhai wa milele.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, kila mtu aliyeacha nyumba au kaka au dada au baba au mama au wana au mashamba kwa ajili ya Jina langu atakapoyapata tena na kuongezwa mara nyingi, kisha ataurithi nao uzima wa kale na kale.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na kila mtu aliyeacha nyumba, au ndugu wa kiume au wa kike, au baba, au mama, au watoto, au mashamba, kwa ajili ya jina langu, atapokea mara mia, na kuurithi uzima wa milele.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na kila mutu aliyeacha nyumba yake, kaka, dada, baba, mama, watoto au mashamba kwa ajili yangu, atapokea mara nyingi zaidi na kupewa uzima wa milele.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na killa mtu aliyeacha nyumba, au ndugu waume, au ndugu wake, au baba, au mama, au watoto, au mashamba, kwa ajili ya jina langu, atapokea marra mia, na kurithi uzima wa milele.