Matthew 2:11 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, wakaingia nyumbani, wakamwona yule mtoto pamoja na Maria mama yake; wakapiga magoti, wakamsujudia. Kisha wakafungua hazina zao, wakampa zawadi: Dhahabu, ubani na manemane.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Walipoingia ndani ya ile nyumba, wakamwona mtoto pamoja na Mariamu mama yake, wakamsujudia na kumwabudu yule mtoto Isa. Ndipo wakafungua hazina zao, wakamtolea zawadi za dhahabu, uvumba na manemane.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wakaingia nyumbani, wakamwona mtoto pamoja na Mariamu mamaye, wakaanguka wakamsujudia; nao walipokwisha kufungua hazina zao, wakamtolea tunu; dhahabu na uvumba na manemane.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Wenye hekima hao kisha waliingia katika nyumba alimokuwamo mtoto Yesu pamoja na Mariamu mama yake. Walisujudu na kumwabudu mtoto. Kisha wakafungua masanduku yenye zawadi walizomletea mtoto. Wakampa hazina za dhahabu, uvumba na manemane.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, wakaingia nyumbani, wakamwona yule mtoto pamoja na Maria mama yake; wakapiga magoti, wakamsujudia. Kisha wakafungua hazina zao, wakampa zawadi: dhahabu, ubani na manemane.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, wakaingia nyumbani, wakamwona yule mtoto pamoja na Maria mama yake; wakapiga magoti, wakamsujudia. Kisha wakafungua hazina zao, wakampa zawadi: dhahabu, ubani na manemane.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Walipoingia ndani ya ile nyumba, wakamwona mtoto pamoja na Maria mama yake, wakamsujudu na kumwabudu yule mtoto Yesu. Ndipo wakafungua hazina zao, wakamtolea zawadi za dhahabu, uvumba na manemane.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Walipoingia ndani ya ile nyumba, wakamwona mtoto pamoja na Mariamu mama yake, wakamsujudu na kumwabudu yule mtoto Isa. Ndipo wakafungua hazina zao, wakamtolea zawadi za dhahabu, uvumba na manemane.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wakaingia nyumbani, wakamwona mtoto pamoja na Mariamu mamaye, wakaanguka wakamsujudia; nao walipokwisha kufungua hazina zao, wakamtolea tunu; dhahabu, uvumba na manemane.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, wakaingia nyumbani, wakamwona yule mtoto pamoja na Maria mama yake; wakapiga magoti, wakamsujudia. Kisha wakafungua hazina zao, wakampa zawadi: Dhahabu, ubani na manemane.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wakaingia nyumbani mle, wakamwona mtoto pamoja na mama yake Maria, wakamwangukia na kumnyenyekea. Walipokwisha wakayafungua malimbiko yao, wakamtolea mtoto tunu, dhahabu na uvumba na manemane.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wakaingia nyumbani, wakamwona mtoto pamoja na Mariamu mamaye, wakaanguka wakamsujudia; nao walipokwisha kufungua hazina zao, wakamtolea tunu; dhahabu na uvumba na manemane.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakaingia ndani ya nyumba, wakamwona mutoto pamoja na mama yake, Maria. Wakapiga magoti na kumwabudu mutoto. Kisha wakafungua mizigo yao na kumutolea zawadi ya zahabu, ubani na marasi.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Wakaingia nyumbani, wakamwona mtoto pamoja na Mariamu mama yake, wakaanguka wakasujudu; nao walipokwisha kufungua hazina zao, wakamtolea tumi, dhahabu, uvumba, na manemane.