Matthew 2:18 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Sauti imesikika huko Rama, kilio na maombolezo mengi. Raheli anawalilia watoto wake, wala hataki kutulizwa, maana wote wamefariki.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Sauti ilisikika huko Rama, maombolezo na kilio kikubwa, Raheli akilia kwa ajili ya wanawe, akikataa kufarijiwa, kwa sababu hawako tena.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Sauti ilisikiwa Rama, Kilio, na maombolezo mengi, Raheli akiwalilia watoto wake, Asikubali kufarijiwa, kwa kuwa hawako.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
“Sauti imesikika Rama, sauti ya kilio na huzuni kuu. Raheli akiwalilia watoto wake, na amekataa kufarijiwa kwa sababu watoto wake hawapo tena.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
“Sauti imesikika mjini Rama, kilio na maombolezo mengi. Raheli anawalilia watoto wake, wala hataki kutulizwa, maana wote wamefariki.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Sauti imesikika huko Rama, kilio na maombolezo mengi. Raheli anawalilia watoto wake, wala hataki kutulizwa, maana wote wamefariki.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Sauti ilisikika huko Rama, kilio cha huzuni na maombolezo makuu, Raheli akilia kwa ajili ya wanawe, akikataa kufarijiwa, kwa sababu hawako tena.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Sauti ilisikika huko Rama, maombolezo na kilio kikubwa, Raheli akilia kwa ajili ya wanawe, akikataa kufarijiwa, kwa sababu hawako tena.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Sauti ilisikiwa Rama, Kilio na maombolezo mengi, Raheli akiwalilia watoto wake, Asikubali kufarijiwa, kwa kuwa hawapo tena.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Sauti imesikika huko Rama, kilio na maombolezo mengi. Raheli anawalilia watoto wake, wala hataki kutulizwa, maana wote wamefariki.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Sauti imesikiwa Rama, ni kilio na maombolezo mengi. Raheli anawalilia watoto wake, hakutaka kubembelezwa, kwani hawako.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Sauti ilisikiwa Rama, Kilio, na maombolezo mengi, Raheli akiwalilia watoto wake, Asikubali kufarijiwa, kwa kuwa hawako.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Sauti inasikilika toka Rama, kilio na malalamiko mengi. Ni Rakeli anayewalilia watoto wake, naye hataki kufarijiwa, kwa maana hawako tena.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Sauti ilisikiwa Rama, Kilio, na kulalama, na maombolezo, Rahel akiwalilia watoto wake, Asikubali kufarijiwa, maana hawako.