Matthew 2:22 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini Yosefu aliposikia kwamba Arkelao, mwanawe Herode, alikuwa mfalme wa Yudea mahali pa baba yake, aliogopa kwenda huko. Naye, baada ya kuonywa katika ndoto, alikwenda pande za Galilaya,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini aliposikia kwamba Arkelao alikuwa anatawala huko Yudea baada ya Herode baba yake, aliogopa kwenda huko. Kwa kuwa alikuwa ameonywa katika ndoto, akaenda zake sehemu za Galilaya,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini aliposikia ya kwamba Arkelao anamiliki huko Uyahudi mahali pa Herode babaye, aliogopa kwenda huko; naye akiisha kuonywa katika ndoto, akasafiri pande za Galilaya,
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Lakini Yusufu aliposikia kuwa Arkelao alikuwa mfalme wa Yuda baada ya baba yake kufa, aliogopa kwenda huko. Lakini baada ya kuonywa na Mungu katika ndoto, Yusufu aliondoka pamoja na familia yake akaenda sehemu za Galilaya.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Lakini Yosefu aliposikia kwamba Arkelao mwanawe Herode alikuwa mfalme wa Yudea mahali pa baba yake, aliogopa kwenda huko. Naye baada ya kuonywa katika ndoto, alikwenda katika mkoa wa Galilaya,
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini Yosefu aliposikia kwamba Arkelao, mwanawe Herode, alikuwa mfalme wa Yudea mahali pa baba yake, aliogopa kwenda huko. Naye, baada ya kuonywa katika ndoto, alikwenda pande za Galilaya,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini aliposikia kwamba Arkelao alikuwa anatawala huko Uyahudi mahali pa Herode baba yake, aliogopa kwenda huko. Naye akiisha kuonywa katika ndoto, akaenda zake sehemu za Galilaya,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini aliposikia kwamba Arkelao alikuwa anatawala huko Uyahudi mahali pa Herode baba yake, aliogopa kwenda huko. Naye akiisha kuonywa katika ndoto, akaenda zake sehemu za Galilaya,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini aliposikia ya kwamba Arkelao anatawala huko Yudea mahali pa Herode babaye, aliogopa kwenda huko; naye akiisha kuonywa katika ndoto, akaenda pande za Galilaya,
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini Yosefu aliposikia kwamba Arkelao, mwanawe Herode, alikuwa mfalme wa Yudea mahali pa baba yake, aliogopa kwenda huko. Naye, baada ya kuonywa katika ndoto, alikwenda pande za Galilaya,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini aliposikia, ya kuwa Arkelao ametawala Yudea mahali pa Herode, baba yake, akaogopa kwenda huko. Basi akaagizwa kwa ndoto, aende zake pande za Galilea;
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini aliposikia ya kwamba Arkelao anamiliki huko Uyahudi mahali pa Herode babaye, aliogopa kwenda huko; naye akiisha kuonywa katika ndoto, akasafiri pande za Galilaya,
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini aliposikia kwamba Arkelao alitawala katika jimbo la Yudea kwa pahali pa baba yake Herode, Yosefu akaogopa kwenda kule. Na alipokwisha kuonywa katika ndoto, akaenda katika jimbo la Galilaya.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Lakini aliposikia ya kwamba Arkelao anamiliki Yahudi mahali pa Herode baba yake, akaogopa kwenda huko; akaonywa katika ndoto, akaenda zake hatta pande za Galilaya,