Matthew 2:8 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha akawatuma Bethlehemu akisema, “Nendeni mkachunguze kwa makini habari za mtoto huyo. Mkisha mpata nileteeni habari ili nami niende kumwabudu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha akawatuma Bethlehemu na kuwaambia, “Nendeni mkamtafute mtoto huyo kwa makini. Mara tu mtakapompata, nileteeni taarifa ili nami niende kumwabudu.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akawapeleka Bethlehemu, akasema, Shikeni njia, mkaulize sana mambo ya mtoto; na mkiisha kumwona, nileteeni habari, ili mimi nami niende nimsujudie.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kisha akawaruhusu waende Bethlehemu. Akawaambia, “Nendeni mkamtafute mtoto kwa makini na mtakapompata mrudi na kunipa taarifa mahali alipo, ili nami pia niende kumwabudu.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kisha akawatuma Bethlehemu akisema, “Nendeni mkachunguze kwa makini habari za mtoto huyo. Mkisha mpata nileteeni habari ili nami niende nikamwabudu.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha akawatuma Bethlehemu akisema, “Nendeni mkachunguze kwa makini habari za mtoto huyo. Mkisha mpata nileteeni habari ili nami niende kumwabudu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha akawatuma waende Bethlehemu akiwaambia, “Nendeni mkamtafute kwa bidii huyo mtoto. Nanyi mara mumwonapo, mniletee habari ili na mimi niweze kwenda kumwabudu.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha akawatuma waende Bethlehemu akiwaambia, “Nendeni mkamtafute kwa bidii huyo mtoto. Nanyi mara mtakapomwona, mniletee habari ili na mimi niweze kwenda kumwabudu.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akawatuma Bethlehemu, akasema, Nendeni mkachunguze kwa makini habari za mtoto; na mkiisha kumwona, nileteeni habari, ili mimi nami niende nimsujudie.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha akawatuma Bethlehemu akisema, “Nendeni mkachunguze kwa makini habari za mtoto huyo. Mkisha mpata nileteeni habari ili nami niende kumwabudu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Akawatuma Beti-Lehemu akisema: Nendeni, mkapeleleze sana habari za mtoto huyo! Mtakapomwona mnipashe habari, nami nipate kwenda nimwangukie.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akawapeleka Bethlehemu, akasema, Shikeni njia, mkaulize sana mambo ya mtoto; na mkiisha kumwona, nileteeni habari, ili mimi nami niende nimsujudie.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha akawatuma Betelehemu, akiwaambia: “Mwende mupeleleze habari kamili za mutoto yule. Nanyi mutakapomwona munijulishe kusudi mimi vilevile niende kumwabudu.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Akawapeleka Bethlehemu, akasema, Shikeni njia, mkahoji sana mambo ya mtoto; mkiisha kumwona, nileteeni khabari, illi nami nije nimsujudie.