Matthew 2:9 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Baada ya kumsikiliza mfalme, hao wataalamu wa nyota wakaenda. Kumbe ile nyota waliyokuwa wameiona upande wa mashariki iliwatangulia hata ikaenda kusimama juu ya mahali pale alipokuwa mtoto.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Baada ya kumsikia mfalme, wale wataalamu wa nyota wakaenda zao, nayo ile nyota waliyoiona mashariki ikawatangulia, nao wakaifuata hadi iliposimama mahali alipokuwa mtoto.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nao waliposikia maneno ya mfalme, walishika njia; na tazama, ile nyota waliyoiona mashariki ikawatangulia, hata ikaenda ikasimama juu ya mahali alipokuwapo mtoto.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Wenye hekima walipomsikiliza mfalme, waliondoka. Waliiona tena ile nyota waliyoiona hapo mwanzo na wakaifuata. Nyota ile iliwaongoza mpaka mahali alipokuwa mtoto na kusimama juu ya sehemu hiyo.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Baada ya kumsikiliza mfalme, hao wataalamu wa nyota wakaenda. Kumbe ile nyota waliyokuwa wameiona upande wa mashariki iliwatangulia hata ikaenda kusimama juu ya mahali pale alipokuwa mtoto.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Baada ya kumsikiliza mfalme, hao wataalamu wa nyota wakaenda. Kumbe ile nyota waliyokuwa wameiona upande wa mashariki iliwatangulia hata ikaenda kusimama juu ya mahali pale alipokuwa mtoto.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Baada ya kumsikia mfalme, wale wataalamu wa nyota wakaenda zao, nayo ile nyota waliyoiona mashariki ikawatangulia, nao wakaifuata mpaka iliposimama mahali pale alipokuwa mtoto.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Baada ya kumsikia mfalme, wale wataalamu wa nyota wakaenda zao, nayo ile nyota waliyoiona mashariki ikawatangulia, nao wakaifuata mpaka iliposimama mahali pale alipokuwa mtoto.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nao waliposikia maneno ya mfalme, walishika njia; na tazama, ile nyota waliyoiona mashariki ikawatangulia, mpaka iliposimama juu ya mahali alipokuwapo mtoto.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Baada ya kumsikiliza mfalme, hao wataalamu wa nyota wakaenda. Kumbe ile nyota waliyokuwa wameiona upande wa mashariki iliwatangulia hata ikaenda kusimama juu ya mahali pale alipokuwa mtoto.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nao walipokwisha msikia mfalme wakashika njia. Walipotazama, ile nyota, waliyoiona maawioni kwa jua, ikawatangulia, mpaka ikaja kusimama juu sawa ya mle alimokuwa yule mtoto.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nao waliposikia maneno ya mfalme, walishika njia; na tazama, ile nyota waliyoiona mashariki ikawatangulia, hata ikaenda ikasimama juu ya mahali alipokuwapo mtoto.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha kumusikiliza mufalme, wakaondoka. Ile nyota waliyoiona tokea mashariki iliwatangulia, nayo ikaenda na kusimama juu ya pahali mutoto alipokuwa.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Nao waliposikia maneno ya mfalme wakashika njia; na tazama ile nyota waliyoiona mashariki ikawatangulia, hatta ikaenda ikasimama juu ya mahali alipokuwapo mtoto.