Matthew 20:12 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakasema, ‘Watu hawa walioajiriwa mwisho walifanya kazi kwa muda wa saa moja tu, mbona umetutendea sawa na wao hali sisi tumevumilia kazi ngumu kutwa na jua kali?’
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
wakisema, ‘Hawa watu walioajiriwa mwisho wamefanya kazi kwa muda wa saa moja tu, nawe umewafanya sawa na sisi ambao tumestahimili taabu na joto lote la mchana kutwa?’
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
wakisema, Hao wa mwisho wametenda kazi saa moja tu, nawe umewasawazisha na sisi tuliostahimili taabu na hari za mchana kutwa.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Walisema, ‘Watu hao walioajiriwa mwishoni wamefanya kazi saa moja tu. Lakini umewalipa sawa na sisi. Na tumefanya kazi siku nzima kwenye jua kali.’
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Wakasema, Watu hawa walioajiriwa mwisho walifanya kazi kwa muda wa saa moja tu, mbona umetutendea sawa na wao hali sisi tumevumilia kazi ngumu kutwa na jua kali?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakasema, ‘Watu hawa walioajiriwa mwisho walifanya kazi kwa muda wa saa moja tu, mbona umetutendea sawa na wao hali sisi tumevumilia kazi ngumu kutwa na jua kali?’
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
wakisema, ‘Hawa watu walioajiriwa mwisho wamefanya kazi kwa muda wa saa moja tu, nawe umewafanya sawa na sisi ambao tumestahimili taabu na joto lote la mchana kutwa?’
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
wakisema, ‘Hawa watu walioajiriwa mwisho wamefanya kazi kwa muda wa saa moja tu, nawe umewafanya sawa na sisi ambao tumestahimili taabu na joto lote la mchana kutwa?’
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
wakisema, Hao wa mwisho wamefanya kazi saa moja tu, nawe umewasawazisha na sisi tuliostahimili taabu na joto la mchana kutwa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wakasema, ‘Watu hawa walioajiriwa mwisho walifanya kazi kwa muda wa saa moja tu, mbona umetutendea sawa na wao hali sisi tumevumilia kazi ngumu kutwa na jua kali?’
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
wakisema: Hawa wa mwisho wamefanya kazi saa moja tu, nawe umewalinganisha na sisi tuliosumbuka kwa kazi na kwa jua kali mchana kutwa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
wakisema, Hao wa mwisho wametenda kazi saa moja tu, nawe umewasawazisha na sisi tuliostahimili taabu na hari za mchana kutwa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakasema: ‘Watumishi hawa wa mwisho wametumika kazi kwa saa moja tu, nawe umewalipa sawasawa na sisi tuliovumilia muchoko na jua kali kwa muchana kutwa!’
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
wakinena, Hawa wa mwisho wametenda kazi saa moja tu, nawe umewasawazisha na sisi tuliostahimili taabu na hari za mchana.