Matthew 20:17 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yesu alipokuwa anakwenda juu Yerusalemu, aliwachukua wale wanafunzi kumi na wawili faraghani, na njiani akawaambia,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Basi Isa alipokuwa anapanda kwenda Yerusalemu, aliwaita kando wale wanafunzi kumi na wawili na kuwaambia,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hata Yesu alipokuwa akipanda kwenda Yerusalemu, aliwachukua wale wanafunzi kumi na wawili faraghani; na njiani akawaambia,
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Yesu alikuwa anakwenda Yerusalemu akiwa na wafuasi wake kumi na wawili. Walipokuwa wakitembea, aliwakusanya pamoja wafuasi hao na kuzungumza nao kwa faragha. Akawaambia,
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Yesu alipokuwa anakwenda Yerusalemu, aliwachukua wale wanafunzi kumi na wawili faraghani, na njiani akawaambia,
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yesu alipokuwa anakwenda juu Yerusalemu, aliwachukua wale wanafunzi kumi na wawili faraghani, na njiani akawaambia,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Basi Yesu alipokuwa anapanda kwenda Yerusalemu, aliwachukua kando wale wanafunzi wake kumi na wawili na kuwaambia,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Basi Isa alipokuwa anapanda kwenda Yerusalemu, aliwachukua kando wale wanafunzi wake kumi na wawili na kuwaambia,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Yesu alipokuwa akipanda kwenda Yerusalemu, aliwachukua wale wanafunzi kumi na wawili faraghani; na njiani akawaambia,
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yesu alipokuwa anakwenda juu Yerusalemu, aliwachukua wale wanafunzi kumi na wawili faraghani, na njiani akawaambia,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Yesu alipotaka kupanda kwenda Yerusalemu akawachukua wale kumi na wawili, wawe peke yao. Akawaambia njiani:
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hata Yesu alipokuwa akipanda kwenda Yerusalemu, aliwachukua wale wanafunzi kumi na wawili faraghani; na njiani akawaambia,
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yesu alipokuwa katika njia kwenda Yerusalema, akaita wanafunzi wake kumi na wawili pembeni, akawaambia:
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Hatta Yesu alipokuwa akipanda kwenda Yerusalemi, aliwachukua wanafunzi thenashara kwa faragha njiani, akawaambia,