Matthew 20:28 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Jinsi hiyohiyo, Mwana wa Mtu hakuja kutumikiwa, bali kutumikia na kutoa maisha yake kuwa fidia ya watu wengi.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
kama vile Mwana wa Adamu hakuja kutumikiwa, bali kutumika na kuutoa uhai wake uwe fidia kwa ajili ya wengi.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
kama vile Mwana wa Adamu asivyokuja kutumikiwa, bali kutumika, na kutoa nafsi yake iwe fidia ya wengi.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Fanyeni kama nilivyofanya: Mwana wa Adamu hakuja ili atumikiwe na watu. Alikuja ili awatumikie wengine na kutoa maisha yake ili kuwaokoa watu wengi.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Jinsi hiyohiyo, Mwana wa Mtu hakuja kutumikiwa, bali kutumikia na kutoa maisha yake kuwa fidia ya watu wengi.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Jinsi hiyohiyo, Mwana wa Mtu hakuja kutumikiwa, bali kutumikia na kutoa maisha yake kuwa fidia ya watu wengi.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
kama vile ambavyo Mwana wa Adamu hakuja ili kutumikiwa, bali kutumika na kuutoa uhai wake uwe fidia kwa ajili ya wengi.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
kama vile ambavyo Mwana wa Adamu hakuja ili kutumikiwa, bali kutumika na kuutoa uhai wake uwe fidia kwa ajili ya wengi.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
kama vile Mwana wa Adamu asivyokuja kutumikiwa, bali kutumika, na kutoa nafsi yake iwe fidia ya wengi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Jinsi hiyohiyo, Mwana wa Mtu hakuja kutumikiwa, bali kutumikia na kutoa maisha yake kuwa fidia ya watu wengi.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kama Mwana wa mtu asivyokuja, atumikiwe, ila amekuja kutumika na kuitoa roho yake kuwa makombozi ya watu wengi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
kama vile Mwana wa Adamu asivyokuja kutumikiwa, bali kutumika, na kutoa nafsi yake iwe fidia ya wengi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa maana Mwana wa Mutu hakukuja kutumikiwa, lakini kutumikiana na kutoa maisha yake kusudi awakomboe watu wengi.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
kama vile Mwana wa Adamu asivyokuja kukhudumiwa, bali kukhudumu, na kutoa roho yake kuwa dia ya wengi.