Matthew 20:30 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, kulikuwa na vipofu wawili wameketi kando ya njia, na waliposikia kwamba Yesu alikuwa anapitia hapo, walipaza sauti: “Bwana, Mwana wa Daudi, utuhurumie!”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Vipofu wawili walikuwa wameketi kando ya barabara. Waliposikia kwamba Isa alikuwa anapita, wakapaza sauti wakisema, “Bwana Isa, Mwana wa Daudi, tuhurumie!”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na tazama, vipofu wawili wameketi kando ya njia, nao waliposikia ya kwamba Yesu anapita, walipaza sauti, wakisema, Uturehemu, Bwana, mwana wa Daudi!
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Walikuwepo wasiyeona wawili wamekaa kando ya njia. Waliposikia kuwa Yesu anapita pale walipaza sauti wakasema, “Bwana, Mwana wa Daudi, tafadhali tusaidie!”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, kulikuwa na vipofu wawili wameketi kando ya njia, na waliposikia kwamba Yesu alikuwa anapitia hapo, walipaaza sauti: “Mheshimiwa, Mwana wa Daudi, utuhurumie!”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, kulikuwa na vipofu wawili wameketi kando ya njia, na waliposikia kwamba Yesu alikuwa anapitia hapo, walipaza sauti: “Bwana, Mwana wa Daudi, utuhurumie!”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Vipofu wawili walikuwa wameketi kando ya barabara. Waliposikia kwamba Yesu alikuwa anapita, wakapiga kelele wakisema, “Bwana, Mwana wa Daudi, uturehemu!”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Vipofu wawili walikuwa wameketi kando ya barabara. Waliposikia kwamba Isa alikuwa anapita, wakapiga kelele wakisema, “Bwana Isa, Mwana wa Daudi, tuhurumie!”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na tazama, vipofu wawili walikuwa wameketi kando ya njia, nao waliposikia ya kwamba Yesu anapita, walipaza sauti, wakisema, Uturehemu, Bwana, mwana wa Daudi!
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, kulikuwa na vipofu wawili wameketi kando ya njia, na waliposikia kwamba Yesu alikuwa anapitia hapo, walipaza sauti: “Bwana, Mwana wa Daudi, utuhurumie!”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, vipofu wawili waliokaa njani kando waliposikia, ya kuwa ni Yesu anayepita, wakapaza sauti wakisema: Bwana, mwana wa Dawidi, tuhurumie!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na tazama, vipofu wawili wameketi kando ya njia, nao waliposikia ya kwamba Yesu anapita, walipaza sauti, wakisema, Uturehemu, Bwana, mwana wa Daudi!
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na kulikuwa vipofu wawili waliokuwa wakiikaa pembeni ya njia, nao wakasikia kwamba Yesu anapita. Kwa hiyo wakalalamika, wakisema: “Bwana, mwana wa Daudi, utusikilie huruma!”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na vipofu wawili wameketi kando ya njia, nao waliposikia ya kwamba Yesu anapita, wakapaaza sauti zao, wakinena, Uturehemu, Ee Bwana, mwana wa Daud!