Matthew 20:6 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hata mnamo saa kumi na moja jioni, akatoka tena; akakuta watu wengine wamesimama pale sokoni. Basi, akawauliza, ‘Mbona mmesimama hapa mchana kutwa bila kazi?’
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mnamo saa kumi na moja akatoka tena akawakuta wengine bado wamesimama bila kazi. Akawauliza, ‘Kwa nini mmesimama hapa kutwa nzima pasipo kufanya kazi?’
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hata kama saa kumi na moja akatoka, akakuta wengine wamesimama, akawaambia, Mbona mmesimama hapa mchana kutwa bila kazi?
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Ilipofika saa kumi na moja alikwenda sokoni tena. Akawaona watu wengine wamesimama pale. Akawauliza, ‘Kwa nini mmesimama hapa siku nzima na hamfanyi kazi?’
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Hata mnamo saa kumi na moja jioni, akatoka tena; akakuta watu wengine wamesimama pale sokoni. Basi, akawauliza, Mbona mmesimama hapa mchana kutwa bila kazi?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hata mnamo saa kumi na moja jioni, akatoka tena; akakuta watu wengine wamesimama pale sokoni. Basi, akawauliza, ‘Mbona mmesimama hapa mchana kutwa bila kazi?’
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mnamo saa kumi na moja akatoka tena akawakuta wengine bado wamesimama bila kazi. Akawauliza, ‘Kwa nini mmesimama hapa kutwa nzima pasipo kufanya kazi?’
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mnamo saa kumi na moja akatoka tena akawakuta wengine bado wamesimama bila kazi. Akawauliza, ‘Kwa nini mmesimama hapa kutwa nzima pasipo kufanya kazi?’
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hata kama saa kumi na moja akatoka, akakuta wengine wamesimama, akawaambia, Mbona mmesimama hapa mchana kutwa bila kazi?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hata mnamo saa kumi na moja jioni, akatoka tena; akakuta watu wengine wamesimama pale sokoni. Basi, akawauliza, ‘Mbona mmesimama hapa mchana kutwa bila kazi?’
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hata ilipopata saa kumi na moja, akatoka, akaona wengine waliosimama, akawaambia: Mnasimamaje hapa mchana kutwa pasipo kazi?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hata kama saa kumi na moja akatoka, akakuta wengine wamesimama, akawaambia, Mbona mmesimama hapa mchana kutwa bila kazi?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Karibu na saa kumi na moja akatoka tena, naye akakuta watu wengine wakisimama pale kwenye nafasi ile. Akawauliza: ‘Sababu gani munasimama bure hapa muchana kutwa?’
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Hatta mnamo saa edashara akatoka, akakuta wengine wakisimama wasiokuwa na kazi, akawaambia, Mbona mmesimama hapa mchana kutwa bila kazi?