Matthew 21:15 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, makuhani wakuu na waalimu wa sheria walipoyaona maajabu aliyoyafanya Yesu, na pia watoto walipokuwa wanapaza sauti zao hekaluni wakisema: “Sifa kwa Mwana wa Daudi,” wakakasirika.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini viongozi wa makuhani na walimu wa Torati walipoona mambo ya ajabu aliyofanya, na kuwasikia watoto wakishangilia katika eneo la Hekalu, wakisema, “Hosana Mwana wa Daudi,” walikasirika.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini wakuu wa makuhani na waandishi walipoyaona maajabu aliyoyafanya, na watoto waliopaza sauti zao hekaluni, wakisema, Hosana, Mwana wa Daudi! Walikasirika,
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Viongozi wa makuhani na walimu wa sheria waliona mambo ya ajabu aliyokuwa anatenda. Na waliona watoto walivyokuwa wanamsifu wakisema, “Sifa kwa Mwana wa Daudi.” Mambo haya yote yaliwakasirisha makuhani na walimu wa sheria.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Basi, makuhani wakuu na walimu wa Sheria walipoyaona maajabu aliyoyafanya Yesu, na pia watoto walipokuwa wanapaaza sauti zao Hekaluni wakisema: “Sifa kwa Mwana wa Daudi,” wakakasirika.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, makuhani wakuu na waalimu wa sheria walipoyaona maajabu aliyoyafanya Yesu, na pia watoto walipokuwa wanapaza sauti zao hekaluni wakisema: “Sifa kwa Mwana wa Daudi,” wakakasirika.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini viongozi wa makuhani na walimu wa sheria walipoona mambo ya ajabu aliyofanya na kuwasikia watoto wakishangilia katika eneo la Hekalu wakisema, “Hosana Mwana wa Daudi”, walikasirika.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini viongozi wa makuhani na walimu wa Torati walipoona mambo ya ajabu aliyofanya na kuwasikia watoto wakishangilia katika eneo la Hekalu wakisema, “Hosana Mwana wa Daudi,” walikasirika.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini wakuu wa makuhani na waandishi walipoyaona maajabu aliyoyafanya, na watoto waliopaza sauti zao hekaluni, wakisema, Hosana, Mwana wa Daudi! Walikasirika,
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, makuhani wakuu na waalimu wa sheria walipoyaona maajabu aliyoyafanya Yesu, na pia watoto walipokuwa wanapaza sauti zao hekaluni wakisema: “Sifa kwa Mwana wa Daudi,” wakakasirika.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini watambikaji wakuu na waandishi walipoyaona mataajabu, aliyoyafanya, tena waliposikia, watoto wakipaza sauti hapo Patakatifu na kusema: Hosiana, mwana wa Dawidi! ndipo, walipokasirika,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini wakuu wa makuhani na waandishi walipoyaona maajabu aliyoyafanya, na watoto waliopaza sauti zao hekaluni, wakisema, Hosana, Mwana wa Daudi! Walikasirika,
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini wakubwa wa makuhani na walimu wa Sheria wakachukizwa kwa kuona miujiza aliyoifanya na watoto waliokuwa wakilalamika katika hekalu, wakisema: “Usifiwe wewe, mwana wa Daudi!”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Lakini makuhani wakuu na waandishi walipoyaona maajabu aliyoyafanya, na watoto wakipaaza sauti zao hekaluni, wakinena, Utuokoe sasa, mwana wa Daud! wakakasirika,