Matthew 21:16 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hivyo wakamwambia, “Je, husikii wanachosema?” Yesu akawajibu, “Naam, nasikia! Je hamjapata kusoma Maandiko haya? ‘Kwa vinywa vya watoto wadogo na wachanga wajipatia sifa kamili.’”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wakamuuliza Isa, “Je, unasikia hayo hawa wanayosema?” Akawajibu, “Naam; kwani hamkusoma, “ ‘Midomoni mwa watoto wachanga na wanaonyonya umeamuru sifa’?”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
wakamwambia, Wasikia hawa wasemavyo? Yesu akawaambia, Naam; hamkupata kusoma, Kwa vinywa vya watoto wachanga na wanyonyao umekamilisha sifa?
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Wakamwuliza Yesu, “Unasikia wanayosema watoto hawa?” Akajibu, “Ndiyo. Maandiko yanasema, ‘Umewafundisha watoto wadogo na watoto wanyonyao kusifu.’ Hamjasoma Maandiko haya?”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Hivyo wakamwambia, “Je, husikii wanachosema?” Yesu akawajibu, “Naam, nasikia! Je hamjasoma Maandiko haya Matakatifu? Kwa vinywa vya watoto wadogo na wanyonyao unajipatia sifa kamilifu.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hivyo wakamwambia, “Je, husikii wanachosema?” Yesu akawajibu, “Naam, nasikia! Je hamjapata kusoma Maandiko haya? ‘Kwa vinywa vya watoto wadogo na wachanga wajipatia sifa kamili.’”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakamwuliza Yesu, “Je, unasikia hayo hawa wanayosema?” Akawajibu, “Naam; kwani hamkusoma, “ ‘Kutoka katika vinywa vya watoto wachanga na wale wanaonyonya umeamuru sifa kamili?’ ”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakamuuliza Isa, “Je, unasikia hayo hawa wanayosema?” Akawajibu, “Naam; kwani hamkusoma, “ ‘Midomoni mwa watoto wachanga na wanyonyao umeamuru sifa’?”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
wakamwambia, Wasikia hawa wasemavyo? Yesu akawaambia, Naam; hamkupata kusoma, Kwa vinywa vya watoto wachanga na wanyonyao umejiandalia sifa?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hivyo wakamwambia, “Je, husikii wanachosema?” Yesu akawajibu, “Naam, nasikia! Je hamjapata kusoma Maandiko haya? ‘Kwa vinywa vya watoto wadogo na wachanga wajipatia sifa kamili.’”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
wakamwambia: Unasikia, hawa wanavyosema? Yesu akawaambia: Ndio. Hamjalisoma bado neno lile la kwamba: Vinywani mwao watoto wachanga namo mwao wanyonyao ulitengeneza tukuzo?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
wakamwambia, Wasikia hawa wasemavyo? Yesu akawaambia, Naam; hamkupata kusoma, Kwa vinywa vya watoto wachanga na wanyonyao umekamilisha sifa?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi wakamwuliza Yesu: “Unasikia maneno watoto hawa wanayoyasema?” Yesu akawajibu: “Ndiyo. Lakini hamujasoma Maandiko Matakatifu yanayosema: ‘Kwa vinywa vya watoto wadogo hata wale wanaokuwa wachanga umetangaza sifa zako.’ ”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
wakamwambia, Wasikia hawa wanenavyo? Yesu akawaambia, Naam; hamkupata kusoma, Kwa vinywa vya watoto wachanga na wanyonyao umekamilisha sifa?