Matthew 21:19 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Akauona mtini mmoja kando ya njia, akauendea; lakini aliukuta hauna chochote ila majani matupu. Basi, akauambia, “Usizae tena matunda milele!” Papo hapo huo mtini ukanyauka.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Akauona mtini kando ya barabara, naye akaukaribia, lakini hakupata tunda lolote ila majani. Ndipo akauambia, “Wewe usizae matunda tena kamwe!” Papo hapo ule mtini ukanyauka.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akaona mtini mmoja kando ya njia, akauendea, asione kitu juu yake ila majani tu; akauambia, Yasipatikane matunda kwako tangu leo hata milele. Mtini ukanyauka mara.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Aliuona mtini karibu na njia na akaenda kuchuma tini kwenye mti huo. Yalikuwepo maua tu. Hivyo Yesu akauambia mti ule, “Hautazaa matunda tena!” Mtini ukakauka na kufa hapo hapo.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Akauona mtini mmoja kando ya njia, akauendea; lakini aliukuta hauma chochote ila majani matupu. Basi akauambia, “Usizae tena matunda milele!” Papo hapo huo mtini ukanyauka.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Akauona mtini mmoja kando ya njia, akauendea; lakini aliukuta hauna chochote ila majani matupu. Basi, akauambia, “Usizae tena matunda milele!” Papo hapo huo mtini ukanyauka.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Akauona mtini kando ya barabara, akaukaribia lakini hakupata tunda lo lote ila majani. Ndipo akauambia, “Wewe na usizae matunda tena kamwe!” Papo hapo ule mtini ukanyauka.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Akauona mtini kando ya barabara, naye akaukaribia, lakini hakupata tunda lolote ila majani. Ndipo akauambia, “Wewe usizae matunda tena kamwe!” Papo hapo ule mtini ukanyauka.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akaona mtini mmoja kando ya njia, akauendea, asione kitu juu yake ila majani tu; akauambia, Yasipatikane matunda kwako tangu leo hata milele. Mtini ukanyauka mara.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Akauona mtini mmoja kando ya njia, akauendea; lakini aliukuta hauna chochote ila majani matupu. Basi, akauambia, “Usizae tena matunda milele!” Papo hapo huo mtini ukanyauka.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Alipoona mkuyu kando ya njia akauendea, asione kitu kwake, ila majani matupu, akauambia: Kale na kale lisipatikane tena tunda kwako! Mara mkuyu ukawa umenyauka.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akaona mtini mmoja kando ya njia, akauendea, asione kitu juu yake ila majani tu; akauambia, Yasipatikane matunda kwako tangu leo hata milele. Mtini ukanyauka mara.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Akaona muti wa tini pembeni ya njia, akaenda karibu nao, lakini hakuona kitu juu yake isipokuwa majani matupu. Halafu Yesu akaulaani muti ule akisema: “Wewe usitoe tena matunda tangu leo hata milele!” Na pale pale muti ule ukakauka.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Akaona mtini mmoja kando ya njia, akauendea, asione kitu juu yake illa majani tu; akauambia, Yasipatikane matunda kwako tangu leo hatta milele. Mtini ukauyauka marra moja.