Matthew 21:26 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Na tukisema, ‘Yalitoka kwa watu,’ tunaogopa umati wa watu maana wote wanakubali kwamba Yohane ni nabii.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini tukisema, ‘Ulitoka kwa wanadamu,’ tunawaogopa hawa watu, maana wote wanamtambua Yahya kuwa ni nabii.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na tukisema, Ulitoka kwa wanadamu, twaogopa mkutano; maana watu wote wamwona Yohana kuwa ni nabii.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Lakini hatuwezi kusema ubatizo wa Yohana ulitoka kwa watu wengine. Tunawaogopa watu, kwa sababu wote wanaamini kuwa Yohana alikuwa nabii.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Na tukisema, Yalitoka kwa watu, tunaogopa umati wa watu maana wote wanakubali kwamba Yohane ni nabii.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Na tukisema, ‘Yalitoka kwa watu,’ tunaogopa umati wa watu maana wote wanakubali kwamba Yohane ni nabii.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini tukisema, ‘Ulitoka kwa wanadamu’, tunawaogopa hawa watu, maana wote wanamtambua Yohana kuwa ni nabii.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini tukisema, ‘Ulitoka kwa wanadamu,’ tunawaogopa hawa watu, maana wote wanamtambua Yahya kuwa ni nabii.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na tukisema, Ulitoka kwa wanadamu, twaogopa mkutano; maana watu wote wamwona Yohana kuwa ni nabii.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Na tukisema, ‘Yalitoka kwa watu,’ tunaogopa umati wa watu maana wote wanakubali kwamba Yohane ni nabii.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini tukisema: Ulitoka kwa watu, tunawaogopa watu; kwani wote wanamshika Yohana kuwa mfumbuaji.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na tukisema, Ulitoka kwa wanadamu, twaogopa mkutano; maana watu wote wamwona Yohana kuwa ni nabii.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini vilevile kwa kuwa tunaogopa watu hawa, hatuwezi kusema kwamba yalitoka kwa mutu; kwa maana watu hawa wote wanasadiki kwamba Yoane alikuwa nabii.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na tukisema, Kwa wana Adamu; twaogopa makutano; maana watu wote wanaona ya kuwa Yohana ni nabii.