Matthew 21:3 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kama mtu akiwauliza sababu, mwambieni, ‘Bwana anawahitaji,’ naye atawaachieni mara.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mtu yeyote akiwasemesha lolote, mwambieni kwamba Bwana ana haja nao, naye atawaruhusu mwalete mara moja.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na kama mtu akiwaambia neno, semeni, Bwana anawahitaji; na mara huyo atawapeleka.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Mtu yeyote akiwauliza kwa nini mnawachukua punda, mwambieni, ‘Bwana anawahitaji. Atawarudisha mapema.’”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Kama mtu akiwauliza sababu, mwambieni, Bwana anawahitaji, naye atawaachieni mara.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kama mtu akiwauliza sababu, mwambieni, ‘Bwana anawahitaji,’ naye atawaachieni mara.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kama mtu ye yote akiwasemesha lo lote, mwambieni kwamba Bwana ana haja nao, naye atawaruhusu mwalete mara.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kama mtu yeyote akiwasemesha lolote, mwambieni kwamba Bwana ana haja nao, naye atawaruhusu mwalete mara.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na kama mtu akiwaambia neno, semeni, Bwana anawahitaji; naye atawatuma mara moja.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kama mtu akiwauliza sababu, mwambieni, ‘Bwana anawahitaji,’ naye atawaachieni mara.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kama mtu atawaambia neno, mwambieni: Bwana wetu anamtakia kazi! mara atawapani.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na kama mtu akiwaambia neno, semeni, Bwana anawahitaji; na mara huyo atawapeleka.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na kama mutu akiwauliza neno, mumwambie kama Bwana yuko na lazima ya kuwatumia. Na mara moja mutu yule atawaruhusu kuwapeleka.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na kama mtu akiwaambieni neno, semeni, Bwana ana haja nao; na marra moja atawapeleka.