Matthew 21:30 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yule baba akamwambia mtoto wake wa pili vivyo hivyo, naye akamjibu, ‘Naam baba!’ Lakini hakuenda kazini.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Kisha yule baba akamwendea yule mwanawe mwingine, akamwambia vilevile. Yeye akajibu, ‘Nitaenda, bwana,’ lakini hakuenda.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Akamwendea yule wa pili, akasema vile vile. Naye akajibu akasema, Sitaki; baadaye akatubu, akaenda.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kisha baba akamwendea mwanaye mwingine na kumwambia, ‘Mwanangu, nenda ukafanye kazi kwenye shamba la mizabibu leo.’ Akajibu, ‘Sawa baba, nitakwenda kufanya kazi.’ Lakini hakwenda.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Yule baba akamwambia mtoto wake wa pili vivyo hivyo, naye akamjibu, Naam baba! Lakini hakwenda kazini.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yule baba akamwambia mtoto wake wa pili vivyo hivyo, naye akamjibu, ‘Naam baba!’ Lakini hakuenda kazini.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Kisha yule baba akamwendea yule mwanawe mwingine akamwambia vile vile. Yeye akajibu, ‘Nitakwenda baba,’ lakini hakwenda.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Kisha yule baba akamwendea yule mwanawe mwingine akamwambia vilevile. Yeye akajibu, ‘Nitakwenda, bwana,’ lakini hakwenda.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Akamwendea yule wa pili, akamwambia vile vile. Naye akajibu akasema, Naenda Bwana; lakini hakuenda.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yule baba akamwambia mtoto wake wa pili vivyo hivyo, naye akamjibu, ‘Naam baba!’ Lakini hakuenda kazini.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Alipomwendea wa pili na kumwambia yaleyale, yeye akajibu akisema: Ndio, bwana; lakini hakuenda.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Akamwendea yule wa pili, akasema vile vile. Naye akajibu akasema, Sitaki; baadaye akatubu, akaenda.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Halafu yule baba akamwambia mutoto wa pili sawa vile alivyomwambia yule wa kwanza. Naye akamujibu: ‘Ndiyo, baba,’ lakini hakwenda.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Akamwendea yule wa pili, akasema vilevile. Nae akajibu akasema, Nakwenda, Bwana: asiende.