Matthew 21:32 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Maana Yohane alikuja kwenu akawaonesha njia adili ya kuishi, nanyi hamkumwamini; lakini watozaushuru na waasherati walimwamini. Hata baada ya kuona hayo yote nyinyi hamkutubu na kumsadiki.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa maana Yahya alikuja kwenu kuwaonesha njia ya haki, lakini hamkumsadiki, lakini watoza ushuru na makahaba wakamsadiki. Nanyi hata mlipoona hayo, baadaye hamkutubu na kumsadiki.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa sababu Yohana alikuja kwenu kwa njia ya haki, ninyi msimwamini; lakini watoza ushuru na makahaba walimwamini, nanyi hata mlipoona, hamkutubu baadaye, ili kumwamini.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Yohana alikuja akiwaonesha njia sahihi ya kuishi, na hamkumwamini. Lakini watoza ushuru na makahaba walimwamini Yohana. Mliona yaliyotokea, lakini hamkubadilika na mlikataa kumwamini.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Maana Yohane alikuja kwenu akawaonyesha njia njema ya kuishi, nanyi hamkumwamini; lakini watoza ushuru na waasherati walimwamini. Hata baada ya kuona hayo yote ninyi hamkubadili mioyo yenu, na hamkusadiki.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Maana Yohane alikuja kwenu akawaonesha njia adili ya kuishi, nanyi hamkumwamini; lakini watozaushuru na waasherati walimwamini. Hata baada ya kuona hayo yote nyinyi hamkutubu na kumsadiki.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa maana Yohana alikuja kwenu kuwaonyesha njia ya haki, lakini hamkumsadiki, lakini watoza ushuru na makahaba wakamsadiki. Nanyi hata mlipoona hayo, baadaye hamkutubu na kumsadiki.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa maana Yahya alikuja kwenu kuwaonyesha njia ya haki, lakini hamkumsadiki, lakini watoza ushuru na makahaba wakamsadiki. Nanyi hata mlipoona hayo, baadaye hamkutubu na kumsadiki.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa sababu Yohana alikuja kwenu kwa njia ya haki, ninyi msimwamini; lakini watoza ushuru na makahaba walimwamini, nanyi hata mlipoona, hamkutubu baadaye, ili kumwamini.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Maana Yohane alikuja kwenu akawaonesha njia adili ya kuishi, nanyi hamkumwamini; lakini watozaushuru na waasherati walimwamini. Hata baada ya kuona hayo yote nyinyi hamkutubu na kumsadiki.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani Yohana alikuja kwenu, akafuata njia yenye wongofu, nanyi hamkumtegemea, lakini watoza kodi na wenye ugoni walimtegemea. Lakini ninyi mlipoviona, hata hapo hamkujuta na kumtegemea.*
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa sababu Yohana alikuja kwenu kwa njia ya haki, ninyi msimwamini; lakini watoza ushuru na makahaba walimwamini, nanyi hata mlipoona, hamkutubu baadaye, ili kumwamini.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa maana Yoane alikuja kwenu kuwaonyesha njia ya haki, nanyi hamukumusadiki. Lakini walipishaji wa kodi na makahaba walimusadiki. Na ijapokuwa muliona mambo hayo yote, hamukugeuka toka zambi zenu na kumusadiki.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Kwa sababu Yohana alikuja kwenu kwa njia ya haki, nanyi hamkumwamini; lakini watoza ushuru na makahaha walimwamini: nanyi mlipoona, hamkutuhu haada ya haya, na kumwamini.