Matthew 21:33 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yesu akasema, “Sikilizeni mfano mwingine. Mtu mmoja mwenye nyumba alilima shamba la mizabibu; akalizungushia ukuta, akachimba kisima cha kusindikia divai, akajenga humo mnara pia. Kisha akalikodisha kwa wakulima, akasafiri kwenda hadi nchi ya mbali.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Sikilizeni mfano mwingine: Kulikuwa na mtu mmoja mwenye shamba ambaye alipanda shamba la mizabibu. Akajenga ukuta kulizunguka, akatengeneza shinikizo la kukamulia zabibu ndani yake, na akajenga mnara wa ulinzi. Kisha akalikodisha hilo shamba la mizabibu kwa wakulima fulani, naye akaondoka, akasafiri hadi nchi nyingine.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Sikilizeni mfano mwingine. Kulikuwa na mtu mwenye nyumba, naye alipanda shamba la mizabibu, akalizungusha ugo, akachimba shimo la shinikizo ndani yake, akajenga mnara, akapangisha wakulima, akasafiri.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Sikilizeni simulizi hii: Alikuwepo mtu aliyemiliki shamba la mizabibu. Alijenga uzio kuzunguka shamba lile la mizabibu na akachimba shimo kwa ajili ya kukamulia zabibu. Kisha akajenga mnara wa lindo. Akalikodisha shamba kwa wakulima kisha akasafiri.
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Yesu akasema, “Sikilizeni mfano mwingine. Mtu mmoja mwenye nyumba alilima shamba la mizabibu; akalizungushia ukuta, akachimba kisima cha kusindikia divai, akajenga humo mnara pia. Kisha akalikodisha kwa wakulima, akasafiri kwenda nchi ya mbali.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yesu akasema, “Sikilizeni mfano mwingine. Mtu mmoja mwenye nyumba alilima shamba la mizabibu; akalizungushia ukuta, akachimba kisima cha kusindikia divai, akajenga humo mnara pia. Kisha akalikodisha kwa wakulima, akasafiri kwenda hadi nchi ya mbali.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Sikilizeni mfano mwingine: Kulikuwa na mtu mmoja mwenye shamba ambaye alipanda mizabibu. Akajenga ukuta kulizunguka, akatengeneza shinikizo ndani yake na akajenga mnara wa ulinzi. Kisha akalikodisha hilo shamba la mizabibu kwa wakulima fulani, naye akaondoka akasafiri kwenda nchi nyingine.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Sikilizeni mfano mwingine: Kulikuwa na mtu mmoja mwenye shamba ambaye alipanda shamba la mizabibu. Akajenga ukuta kulizunguka, akatengeneza shinikizo ndani yake na akajenga mnara wa ulinzi. Kisha akalikodisha hilo shamba la mizabibu kwa wakulima fulani, naye akaondoka, akasafiri kwenda nchi nyingine.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Sikilizeni mfano mwingine. Kulikuwa na mtu mwenye shamba, naye alipanda shamba la mizabibu, akalizungushia ua, akachimba shimo la shinikizo ndani yake, akajenga mnara, akapangisha wakulima, akasafiri.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yesu akasema, “Sikilizeni mfano mwingine. Mtu mmoja mwenye nyumba alilima shamba la mizabibu; akalizungushia ukuta, akachimba kisima cha kusindikia divai, akajenga humo mnara pia. Kisha akalikodisha kwa wakulima, akasafiri kwenda hadi nchi ya mbali.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Sikilizeni mfano mwingine! Kulikuwa na mtu mwenye nyumba aliyepanda mizabibu, akaizungusha ugo, akachimbua humo kamulio la kuzikamulia zabibu, akajenga dungu, akaipangisha wakulima, kisha akaenda katika nchi nyingine.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Sikilizeni mfano mwingine. Kulikuwa na mtu mwenye nyumba, naye alipanda shamba la mizabibu, akalizungusha ugo, akachimba shimo la shinikizo ndani yake, akajenga mnara, akapangisha wakulima, akasafiri.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Musikilize mufano mwingine. Mutu mumoja alipanda shamba la mizabibu, akalizungusha upango, akatengeneza nafasi ya kukamulia matunda ya mizabibu na kujenga munara kwa ajili ya walinzi wa shamba. Kisha kupatana kwa kugawanyana mavuno na walimaji wamoja watakaobaki wakitunza shamba lake, akaenda safari katika inchi ingine.
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Sikilizeni mfano mwingine. Kulikuwa na mtu mwenye nyumba, nae alipanda mizabibu, akazungusha uzio, akachimba shimo ndani yake, akajenga mnara, akapangisha wakulima, akasafiri.