Matthew 21:42 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hapo Yesu akawaambia, “Je, hamkusoma jambo hili katika Maandiko Matakatifu? ‘Jiwe walilokataa waashi sasa limekuwa jiwe kuu la msingi. Bwana ndiye aliyefanya jambo hili, nalo ni la ajabu sana kwetu!’
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Isa akawaambia, “Je, hamjasoma katika Maandiko kwamba: “ ‘Jiwe walilolikataa waashi limekuwa jiwe kuu la pembeni. Mwenyezi Mungu ndiye alitenda jambo hili, nalo ni la kushangaza machoni petu’?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Yesu akawaambia, Hamkupata kusoma katika maandiko, Jiwe walilolikataa waashi, Hilo limekuwa jiwe kuu la pembeni; Neno hili limetoka kwa Bwana, Nalo ni ajabu machoni petu?
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Yesu akawaambia, “Hakika mmesoma hili katika Maandiko: ‘Jiwe walilolikataa waashi limekuwa jiwe kuu la pembeni. Bwana amefanya hivi, na ni ajabu kubwa kwetu kuliona.’
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Hapo Yesu akawaambia, “Je, hamkusoma jambo hili katika Maandiko Matakatifu? Jiwe walilokataa waashi sasa limekuwa jiwe kuu la msingi. Bwana ndiye aliyefanya jambo hili, nalo ni la ajabu sana kwetu!
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hapo Yesu akawaambia, “Je, hamkusoma jambo hili katika Maandiko Matakatifu? ‘Jiwe walilokataa waashi sasa limekuwa jiwe kuu la msingi. Bwana ndiye aliyefanya jambo hili, nalo ni la ajabu sana kwetu!’
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yesu akawaambia, “Je, hamjasoma katika maandiko kwamba: “ ‘Lile jiwe walilolikataa waashi limekuwa jiwe kuu la pembeni; Bwana ndiye aliyefanya jambo hili, nalo ni la ajabu machoni petu’?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Isa akawaambia, “Je, hamjasoma katika Maandiko kwamba: “ ‘Jiwe walilolikataa waashi limekuwa jiwe kuu la pembeni. Bwana Mwenyezi ndiye alitenda jambo hili, nalo ni la ajabu machoni petu’?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Yesu akawaambia, Hamkupata kusoma katika maandiko, Jiwe walilolikataa waashi, Hilo limekuwa jiwe kuu la pembeni; Neno hili limetoka kwa Bwana, Nalo ni la ajabu machoni petu?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hapo Yesu akawaambia, “Je, hamkusoma jambo hili katika Maandiko Matakatifu? ‘Jiwe walilokataa waashi sasa limekuwa jiwe kuu la msingi. Bwana ndiye aliyefanya jambo hili, nalo ni la ajabu sana kwetu!’
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
*Yesu akawaambia: Hamjasoma katika Maandiko ya kuwa: Jiwe, walilolikataa waashi, hilihili limekuwa la pembeni? Hivyo vimefanywa na Bwana; nasi tukivitazama, ni vya kustaajabu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Yesu akawaambia, Hamkupata kusoma katika maandiko, Jiwe walilolikataa waashi, Hilo limekuwa jiwe kuu la pembeni; Neno hili limetoka kwa Bwana, Nalo ni ajabu machoni petu?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Na Yesu akawaambia: “Hamujasoma bado Maandiko Matakatifu yanayosema: ‘Jiwe lililokataliwa na wajengaji limekuwa jiwe kubwa la musingi. Ni Bwana aliyefanya jambo hili, nalo ni ajabu sana kwetu.’
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Yesu akawaambia, Hamkupata kusoma katika maandiko, Jiwe walilolikataa waashi, Hili lilikuwa jiwe kuu la pembeni; Neno hili limetoka kwa Bwana, Nalo ni ajabu machoni petu?