Matthew 21:44 — Compare Translations

13 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Atakayeanguka juu ya jiwe hilo atavunjika vipandevipande; na likimwangukia mtu yeyote, litamponda” (taz. Luka 20:18).
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Yeye aangukaye juu ya jiwe hili atavunjika vipande vipande, lakini yule litakayemwangukia atasagwa kabisa.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye aangukaye juu ya jiwe hilo atavunjika-vunjika; naye ye yote ambaye litamwangukia, litamsaga tikitiki.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Kila aangukaye kwenye jiwe hili atavunjika na litamsaga kila linayemwangukia.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
“Atakayeanguka juu ya jiwe hilo atavunjika vipandevipande; na likimwangukia mtu yeyote, litamponda.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Yeye aangukaye kwenye jiwe hili atavunjika vipande vipande, lakini yule litakayemwangukia atasagika kabisa.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Yeye aangukaye juu ya jiwe hili atavunjika vipande vipande, lakini yule litakayemwangukia atasagwa kabisa.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye aangukaye juu ya jiwe hilo atavunjika vipande vipande; naye yeyote ambaye litamwangukia, litamsaga tikitiki.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Atakayeanguka juu ya jiwe hilo atavunjika vipandevipande; na likimwangukia mtu yeyote, litamponda” (taz. Luka 20:18).
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye atakayeanguka juu ya jiwe hilo atapondeka, naye litakayemwangukia, litambana tikitiki*.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye aangukaye juu ya jiwe hilo atavunjika-vunjika; naye ye yote ambaye litamwangukia, litamsaga tikitiki.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Anayeanguka juu ya jiwe hili atavunjikavunjika, na yule litakayemwangukia, atapondekana.]”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Nae aangukiae juu ya jiwe hili atavunjikavunjika: nae amhae litamwangukia, litampondaponda.