Matthew 21:9 — Compare Translations
14 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Makundi ya watu waliomtangulia na wale waliomfuata wakapaza sauti: “Sifa kwa Mwana wa Daudi! Abarikiwe huyo ajaye kwa jina la Bwana! Sifa kwa Mungu juu!”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wale umati wa watu waliomtangulia na wale waliomfuata wakapaza sauti na kusema, “Hosana, Mwana wa Daudi!” “Amebarikiwa yeye ajaye kwa Jina la Mwenyezi Mungu!” “Hosana juu mbinguni!”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na makutano waliotangulia, na wale waliofuata, wakapaza sauti, wakisema, Hosana, Mwana wa Daudi; ndiye mbarikiwa, yeye ajaye kwa jina la Bwana; Hosana juu mbinguni.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Wengine walimtangulia Yesu, na wengine walikuwa nyuma yake. Wote walipaza sauti wakisema: “Msifuni Mwana wa Daudi! ‘Karibu! Mungu ambariki yeye ajaye katika jina la Bwana!’ Msifuni Mungu wa mbinguni!”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Makundi ya watu waliomtangulia na wale waliomfuata wakapaaza sauti: “Hosana Mwana wa Daudi! Abarikiwe huyo ajaye kwa jina la Bwana! Hosana Mungu juu mbinguni!”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Makundi ya watu waliomtangulia na wale waliomfuata wakapaza sauti: “Sifa kwa Mwana wa Daudi! Abarikiwe huyo ajaye kwa jina la Bwana! Sifa kwa Mungu juu!”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ule umati wa watu uliomtangulia na ule uliomfuata ukapiga kelele ukisema, “Hosana Mwana wa Daudi!” “Amebarikiwa yeye ajaye kwa Jina la Bwana!” “Hosana juu mbinguni!”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ule umati wa watu uliomtangulia na ule uliomfuata ukapiga kelele ukisema, “Hosana, Mwana wa Daudi! ” “Amebarikiwa yeye ajaye kwa Jina la Bwana Mwenyezi Mungu!” “Hosana juu mbinguni!”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na makutano waliotangulia, na wale waliofuata, wakapaza sauti, wakisema, Hosana, Mwana wa Daudi; ndiye mbarikiwa, yeye ajaye kwa jina la Bwana; Hosana juu mbinguni.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Makundi ya watu waliomtangulia na wale waliomfuata wakapaza sauti: “Sifa kwa Mwana wa Daudi! Abarikiwe huyo ajaye kwa jina la Bwana! Sifa kwa Mungu juu!”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
nao wale watu wengi waliomtangulia, nao waliomfuata wakapaza sauti wakisema: Hosiana, mwana wa Dawidi! Na atukuzwe ajaye kwa Jina la Bwana! Hosiana juu mbinguni!*
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na makutano waliotangulia, na wale waliofuata, wakapaza sauti, wakisema, Hosana, Mwana wa Daudi; ndiye mbarikiwa, yeye ajaye kwa jina la Bwana; Hosana juu mbinguni.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nalo kundi la watu waliomutangulia Yesu na lile la watu waliofuata nyuma yake, wakaanza kulalamika, wakisema: “Usifiwe wewe Mwana wa Daudi! Abarikiwe huyu anayekuja kwa jina la Bwana! Mungu asifiwe juu mbinguni!”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Na makutano waliotangulia, na waliofuata, wakapaaza sauti zao, wakinena, Utuokoe sasa, Mwana wa Daud; amebarikiwa ajae kwa jina la Bwana; Utuokoe sasa wewe uliye juu.