Matthew 22:21 — Compare Translations

14 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakamjibu, “Ni ya Kaisari.” Hapo Yesu akawaambia, “Basi, ya Kaisari mpeni Kaisari, na ya Mungu mpeni Mungu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wakamjibu, “Ni vya Kaisari.” Basi Isa akawaambia, “Mpeni Kaisari kilicho cha Kaisari, naye Mungu mpeni kilicho cha Mungu.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wakamwambia, Ni ya Kaisari. Akawaambia, Basi, mlipeni Kaisari yaliyo ya Kaisari, na Mungu yaliyo ya Mungu.
Swahili (TKU) 2017 (Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi)
Wakajibu, “Ni picha ya Kaisari na ni jina la Kaisari.” Ndipo Yesu akawajibu, “Mpeni Kaisari vilivyo vyake na mpeni Mungu vilivyo vyake.”
Swahili 1850 - Biblia Takatifu
Wakamjibu, “Ni vya Kaisari.” Hapo Yesu akawaambia, “Basi, mpeni Kaisari yaliyo yake Kaisari, na Mungu yaliyo yake Mungu.”
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakamjibu, “Ni ya Kaisari.” Hapo Yesu akawaambia, “Basi, ya Kaisari mpeni Kaisari, na ya Mungu mpeni Mungu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakamjibu, “Ni vya Kaisari.” Basi Yesu akawaambia, “Mpeni Kaisari kilicho cha Kaisari, naye Mungu mpeni kilicho cha Mungu.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakamjibu, “Ni vya Kaisari.” Basi Isa akawaambia, “Mpeni Kaisari kilicho cha Kaisari, naye Mungu mpeni kilicho cha Mungu.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wakamwambia, Ni ya Kaisari. Akawaambia, Basi, mpeni Kaisari yaliyo ya Kaisari, na Mungu yaliyo ya Mungu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wakamjibu, “Ni ya Kaisari.” Hapo Yesu akawaambia, “Basi, ya Kaisari mpeni Kaisari, na ya Mungu mpeni Mungu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, alipowaambia: Basi, yaliyo yake Kaisari mtoleeni Kaisari, naye Mungu yaliyo yake Mungu!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wakamwambia, Ni ya Kaisari. Akawaambia, Basi, mlipeni Kaisari yaliyo ya Kaisari, na Mungu yaliyo ya Mungu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakamujibu: “Ni vya Mufalme wa Roma.” Halafu Yesu akawaambia: “Basi mumupe Mufalme wa Roma vinavyokuwa vyake, na Mungu vinavyokuwa vyake.”
Swahili SWZZB1921 (New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921)
Wakamwambia, Ya Kaisari. Akawaambia, Bassi, mlipeni Kaisari yaliyo ya Kaisari, na Mungu yaliyo ya Mungu.